Baba Levo Akashifu Harmonize Kwa Kumpa Anjella Gari Badala ya Kumpeleka Hospitali India

[Picha: Anjella Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Bongo Flava Babalevo amemkashifu mkurugenzi mkuu wa Konde Music W0rldwide Harmonize kwa kumzawadia msanii Anjella gari badala ya kumsaidia kupata matibabu kwa shida ya mguu aliyonayo.

Msanii Anjella amesainiwa chini ya lebo ya Konde Worldwide Music na kwa sasa amepanda ngazi katika muziki na kutamba bongo.

Soma Pia: Country Wizzy na Ibraah Kuja na Wimbo Mpya wa Pamoja

Hapo awali, Harmonize alifichua kuwa Anjella ako na tatizo la mguu ambalo lilikuwa limeathiri utendakazi wake, Harmonize hata hivyo aliahidi kuwa angempeleka Anjella nchini India kusudi apate matibabu.

Kufikia sasa, Anjella bado hajapata matibabu anayohitaji na kwa hivyo anapata ugumu hata akiwa jukwaani.

Babalevo alimkosoa Harmonize kwa kumpa Anjella zawadi ya gari badala ya kutimiza ahadi yake ya kumpa matibabu. Kauli ya Babalevo ilitokea baada ya Harmonize kuwapa zawadi za magari Anjella pamoja na Jose Wamipango ambaye pia ni meneja wa msanii Ibraah kutoka Konde Worldwide Music.

Soma Pia: Marioo Asifia Ustadi Wa Harmonize Katika Kuimba Nyimbo Za Ushairi Mzito

"Mtu anaumwa mguu badala umsaidie kwenda India unaenda kumpa gari used alilokuwa akitumia Kajala," Babalevo aliandika katika ukurasa wake wa Instagram.

Babalevo anajulikana kwa kuwa mfuasi mkubwa wa Diamond Platnumz. Yeye pia ni mkosoaji mkubwa wa wapinzani wote wa Diamond Platnumz ikiwemo Harmonize.

Kauli yake Babalevo iliibua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki. Wapo waliokubalina naye kuwa Anjella anahitaji matibabu ya dharura na wala si zawadi ya gari, huku wengine wakisema kuwa maoni ya Babalevo yalitokana na uhasama alionao na Harmonize.

Leave your comment