Rich Mavoko Awashauri Wasanii Dhidi ya Kununua Watazamaji YouTube

[Picha: Rich Mavoko Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania Rich Mavoko amewashauri wasanii wenzake kuacha kununua watazamaji wa nyimbo zao kwenye mtandao wa YouTube.

Mwimbaji huyo alikuwa akitoa maoni yake kuhusu madai ya hivi karibuni kwamba wanamuziki wa Bongo wananunua watazamaji ili kufanya nyimbo zao zionekane maarufu.

Soma Pia: Rich Mavoko Azungumzia Tofauti Baina yake na Diamond Platnumz

Kulingana na Rich Mavoko, kununua watazamaji na kutumia njia zisizo sawa za ushindani kutamaliza tu taaluma ya mwanamuziki. Alielezea kuwa kununua watazamaji kutamfanya mwanamuziki kuwa maarufu tu kwa muda mfupi.

Alidai kuwa ni kweli kwamba wanamuziki wengine katika tasnia ya burudani wananunua watazamaji. Mavoko alisema kuwa haikuwa mara ya kwanza kukutana na swala la wanamuziki kutumia njia za udanganyifu.

Soma Pia: Rich Mavoko Kuwashirikisha Wasanii wa Kenya Kwenye Albamu Yake Ijayo

Alilazimishwa pia kujibu madai dhidi yake kuwa alinunua watazamaji kwa moja ya nyimbo zake za hivi karibuni. Rich Mavoko alipuuza madai hayo na kusisitiza kwamba kamwe hawezi kununua watazamaji.

"Naona watu wanaongea kuwa hilo suala lipo. Lakini nafikiri ni kujidanganya tu. Still bado una nafasi kitu chako kifike kule kina stahili. Ukieka muziki kama muziki na nambari zako pia zikawafikia watu inaleta furaha. Lakini ukisema una cheat ni kujidanganya na game yako haiwezikua," Rich Mavoko alisema.

Kwa sasa Rich Mavoko yuko jijini Nairobi ambapo anaandaa albamu yake ijayo. Anatarajiwa kushirikiana na wanamuziki wa Kenya kwenye albamu hiyo.

 

Leave your comment