Rich Mavoko Kuwashirikisha Wasanii wa Kenya Kwenye Albamu Yake Ijayo

[Picha: Rich Mavoko Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Bongo Flava Rich Mavoko ametangaza kuwa kwa sasa anashirikiana na wanamuziki kadhaa wa Kenya kwenye nyimbo ambazo zitakuwa kwenye albamu yake ijayo.

Rich Mavoko alidai kwamba ni nadra sana yeye kukuja Nairobi, isipokuwa wakati ambapo ako na mradi wa kufanya. Kwa hivyo, alidai kwamba safari yake ya sasa ya kuja Nairobi ilikuwa kwa sababu ya miradi mingi ya kumuziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Anjella Aachia Wimbo Mpya ‘Sina Bahati’

Hata hivyo, hakufunua majina ya wanamuziki ambao anashirikiana nao lakini alielezea tu kwamba kazi hiyo ilikuwa tayari imeanza.

Rich Mavoko pia alisema kuwa kulikuwa na video kadhaa za nyimbo zake ambazo zilikuwa zikirekodiwa Nairobi. Hapo awali, Mavoko alikuwa Kenya na hata kusainiwa katika Kaka Empire ambayo iko Nairobi, Kenya. Akiwa Kaka Empire, mwimbaji huyo alitoa vibao kama vile ‘Nikija Nairobi’.

Soma Pia: Zuchu Azungumzia Mafanikio Yake Mwaka Mmoja Kwenye WCB

Mkataba kati yake na Kaka EMpire, hata hivyo, ulimalizika na alirejea Tanzania ambapo baadaye alisainiwa kwenye lebo ya rekodi ya WCB. Rich Mavoko hakufunua iwapo kulikuwa na lebo ya rekodi nyuma ya albamu yake ijayo.

Hivi sasa, Rich Mavoko anavuma sana kwenye mtandao na wimbo wake mpya uitwao ‘Nidonoe’ ambao umepokelewa vizuri sana na mashabiki wake.

Rich Mavoko sasa ameingia katika orodha ya wanamuziki mashuhuri ambao wanatarajiwa kutoa albamu zao hivi karibuni. Wanamuziki wengine ambao pia wametangaza kuwa wanafanya kazi kwenye Albamu zao ni pamoja na Alikiba na Diamond.

Leave your comment