Rich Mavoko Azungumzia Tofauti Baina yake na Diamond Platnumz

[Picha: Rich Mavoko Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania Rich Mavoko ameibuka na kuzungumzia tofauti zinazodaiwa kuwa kati yake na Diamond Platnumz. Akiongea wakati wa mahojiano ambayo alifanya akiwa Kenya, Rich Mavoko aliwashangaza wengi alipokiri kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa karibu na Diamond.

Soma Pia: Rich Mavoko Kuwashirikisha Wasanii wa Kenya Kwenye Albamu Yake Ijayo

Kulingana na Rich Mavoko, yeye na Diamond hawajawahi kuwa marafiki kama watu wengi walivyofikiria. Hii ni licha ya kwamba Rich Mavoko kwa wakati mmoja alikwa amesainiwa chini ya lebo ya rekodi ya WCB inayomilikiwa na Diamond.

Rich Mavoko ambaye alikuwa kwenye tasnia ya burudani ya Kitanzania kwa muda mrefu, alikuwa msanii wa kwanza hata hivyo kuondoka WCB. Akiwa WCB Rich Mavoko alitoa baadhi ya nyimbo zake maarufu zilizotamba kwenye anga za burudani ikiwemo ‘Ibaki Story’.

"Hatukuwa washikaji, na hata tulipokuwa kwenye lebo hatukuwahi kuwa marafiki," Rich Mavoko alisema.

Alidokeza pia kuwa tofauti na mtazamo wa watu wengi, yeye hakutafuta WCB kusudi asiniwe huko. Mavoko alisema kuwa Diamond alituma watu kumshawishi ajiunge na WCB.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Chege Amshirikisha Ommy Dimpoz Kwenye Wimbo Mpya ‘Show Time’

"Sikuwahi kumtafuta mtu kufanya naye kazi kwa sababu nilikuwa na kipaji sana. Nilitafutwa na watu wengine ambao yeye aliwatuma, alishindwa kuni-face, I think," Rich Mavoko aliongeza.

Mwanamuziki huyo kwa sasa yuko Kenya ambapo anafanya ziara ya mahojiano katika vyombo vya habari pia anafanya miradi mingine ya muziki.

Leave your comment