Harmonize Amuunga Mkono Linah Licha ya Ugomvi Baina Yao

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi Mtendaji wa Konde Music Worldwide Harmonize hivi karibuni alijitokeza na kumuunga mkono mwanamuziki wa Tanzania Linah licha ya madai kuwa walikuwa na tofauti.

Wawili hao hivi karibuni walizua gumzo mtandaoni baada ya kubishana kwenye mitandao ya kijamii. Katika moja ya taarifa ambazo Linah alichapisha, alikuwa ametumia maneno mazito dhidi ya Harmonize.

Soma Pia: Zuchu Atangaza Ujio wa Tamasha la ‘Zuchu Homecoming’ Mwezi Ujao Zanzibar

Hii ilifanya watu wengi kuamini kwamba wawili hao hawakuwa na uhusiano mzuri na hawakuwa katika mazungumzo. Harmonize, hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii alimuunga mkono Linah katika moja ya maonyesho ambayo alikuwa akifanya.

Mwimbaji huyo wa ‘Sandakalawe’ alimpigia kampeni Linah na kuwataka mashabiki wake kumtazama Linah wakati akiburudisha katiko onyesho hilo.

Harmonize pia alimsifu Linah na kufunua kuwa pia angependa sana kumtazama Linah akiwa jukwaani akiimba. Kulingana na Harmonize, alikuwa akijivunia Linah na kazi ambayo alikuwa akifanya katika tasnia ya muziki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Mpya Zilizoachiwa Bongo Wiki Hii

"Proud of you ndege mnana ..!!!!!!!!!! What a comeback my people's the queen will be live kwenye homa ya @tvetanzania please show her some love. I  can't wait to see this tonight," chapisho la harmoniza lilisoma.

Hapo awali Linah alikuwa amejitokeza na kukana madai kwamba alikuwa akitafuta kiki kwa kumshambulia Harmonize kwenye mitandao ya kijamii. Linah alisisitiza kuwa amefanikiwa kupitia muziki wake na wala sio kiki.

 

Leave your comment