Zuchu Atangaza Ujio wa Tamasha la ‘Zuchu Homecoming’ Mwezi Ujao Zanzibar

 [Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii maarufu wa WCB Zuchu ametangaza kuwa anaanda tamasha liitwalo ‘Zuchu Homecoming’ litakalofanyika Zanzibar tarehe 21 mwezi Agosti, 2021 katika uwanja wa Amani.

Soma Pia: Wasanii 5 Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Kwenye YouTube Tanzania

Zuchu ambaye amekua mmoja wa wanamuziki wenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya burudani ya Tanzania alisema kuwa imekuwa ndoto yake siku zote kurudi Zanzibar alikokulia. Zuchu alieleza kuwa tamasha hilo pia litakuwa njia ya yeye kutoa shukrani kwa mashabiki wake ambao waliomwona wakati alikuwa mchanga kimuziki.

Mwimbaji huyo alifanya mkutano na waandishi wa habari mnamo tarehe 15 mwezi Julai ambapo alitangaza ujio wa tamasha hilo. Zuchu alikuwa ameandamana na mama yake Khadija Kopa na maafisa wengine kutoka lebo ya rekodi ya WCB ikiwemo meneja wake.

Soma Pia: Zuchu Aweka Rekodi Mpya, Afikisha Jumla ya Watazamaji Milioni Mia Mbili Kwenye YouTube

Baada ya mkutano na wanahabari, Zuchu alichapisha taarifa nyingine kwenye ukurasa wake wa mitandao ya kijamii ambapo aliwathamini mashabiki wake na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wake.

"Imekuwa Ndoto Yangu Ya muda mrefu. Lakini leo nimeanza kuuona Mwanga . Naileta wenu #ZUCHUHOMECOMINGnaZANTEL Asanteni Sana Ndugu Waandishi wa habari Kwa kujiunga Na Mimi Kwenye kutangaza Rasmi Show Yangu Kubwa Ya ZUCHU HOMECOMING NA @zanteltanzania show hii itafanyika uwanja wa Amani tarehe 21-august-2021 kaa karibu na page yangu kujua wasanii tutakao ambatana nao kwenye show hii," Chapisho la Zuchu lilisoma.

Zuchu hivi majuzi alisherehekea mafanikio ya watazamaji zaidi ya milioni mia mbili kwenye mtandao wa YouTube.

Nyimbo nyingi ambazo Zuchu ametoa chini ya usimamizi wa WCB zimepokelewa vizuri na mashabiki.

Leave your comment

Top stories

More News