Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video ya ‘Mtaalam’

[Picha: Ralingo]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutokea lebo ya WCB Mbosso ameachia video ya wimbo wake ‘Mtaalam’ iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

Wimbo wa ‘Mtaalam’ ni wimbo wa kwanza kabisa kwenye albamu ya Mbosso inayojulikana kama ‘Definition of Love.

Read Also: Nyimbo Mpya: Diamond Aachia ‘Iyo’ Akiwashirikisha Focalistic, Mapara A Jazz na Ntoshi Gazz

‘Mtaalam’ imeongozwa na Director Kenny kutokea Zoom Extra na Mbosso hajaenda mbali na ujumbe uliopo kwenye wimbo, kwani mwanzoni mwa video hii Mbosso anaonekana akiwa na mpenzi kwenye bustani iliyopendeza wakichombezana na kufurahi kwa pamoja.

Kwenye sehemu ya kwanza ya video, mahadhi yake yanafanana na ya kwenye video ya Lavalava ‘Utatulia’ iliyotoka Januari 28 mwaka 2018 kwani zote zimefanyika kwa bustani huku video zote mbili zikihusisha hasa wahusika wawili tu.

Read Also: Anjella Afichua Wasanii Atakaowashirikisha Kwenye ‘Nobody’ Remix

Baada ya kuchapisha video hii kwenye akaunti yake ya Instagram, mashabiki wengi kutokea nchi mbalimbali kama Kenya, Zambia, Senegal, Marekani na nyinginezo walionesha kupendezwa na alichokifanya Mbosso kwenye video hii.

"Man you never disappoint 100%.Your lyrics are always on point. Love from Kenya" aliandika mdau mmoja wa muziki.

Baadhi ya wachangiaji pia walionesha kufurahi kwani walisubiri video ya wimbo huo kwa muda mrefu, mchangiaji mmoja aliandika "Was waiting for this, finally its here" huku mwingine aliandika kwa kumsifia Mbosso "Ila Mbosso Fundi Jamani. Swahili Nation well presented."

‘Mtaalam’ ni video ya sita kutoka kwenye albamu ya ‘Definition of Love’ video nyingine ambazo tayari zishatoka ni pamoja na ‘Yalah’, ‘Yes’ akishirikiana na Spice Diana kutokea Uganda, ‘Kiss Me’, ‘Baikoko’ akimshirikisha Diamond Platnumz pamoja na ‘Kamseleleko’ aliyoshirikiana na ‘Baba Levo’.

https://www.youtube.com/watch?v=giHgGzX2PAI

Leave your comment