Khadija Kopa Ashukuru WCB Kwa Kumkuza Zuchu Kimuziki

 [Picha: Khadija Kopa| Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki maarafu kutoka Tanzania Khadija Kopa ametoa shukrani kwa lebo ya rekodi ya WCB kwa kumkuza binti yake Zuchu kimuziki. Khadija Kopa ambaye alikuwa akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Zanzibar, alidai kuwa lebo hiyo ya rekodi ilichukua muda mwingi katika kuhakikisha Zuchu alikuwa mwanamuziki bora.

Soma Pia: Nyimbo 5 za Khadija Kopa Zilizompa Hadhii Katika Taarab [Video]

Khadija pia alifunua kuwa ilichukua muda mrefu kabla ya Zuchu kutajwa rasmi kama msanii aliyesainiwa katika lebo ya rekodi ya WCB. Kulingana na Khadija Kopa, muda huo mrefu ambao uliwekwa kwenye mafunzo ya Zuchu ilistahili na hatimaye imezaa matunda.

"Shukani kubwa natoa kwa Wasafi Media kwa kunipokelea, Fella, Babu Tale, haswaa mwanangu Diamond. Nakumbuka nilipompeleka Zuchu nikawaambia huyu ni mtoto wangu. Diamond alikua anashangaa na anaweza kuimba kweli huyu. Nikamwambia anajitahidi kidogo kidogo tu. Hebu msikilize kwanza.

Soma pia: Khadija Kopa Asheherekea Miaka 25 Katika Tasnia Ya Muziki

Nashukuru wamempokea kwa dhati, kwa nia safi. Wamempa nafasi. Ingawa amekaa muda mrefu, lakini muda huo mrefu walikua wanamtengeneza zaidi," Khadija Kopa alisema.

Khadija na Diamond Platnumz wako na uhusiano mwema ambao umedumu kwa muda mrefu. Wawili hao walishirikiana kwenye wimbo uitwao ‘Nasema Nawe’ takriban miaka sita iliyopita.

Wimbo huo hadi sasa una watazamaji takriban milioni thelathini kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment

Top stories

More News