Diamond Platnumz Akutana na Snoop Dogg Katika Ziara yake Marekani

 [Picha: Diamond Platnumz | Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota wa Tanzania Diamond Platnumz anaendelea kuongeza umaarufu wake huko Marekani kwa kukutana na mastaa mbali mbali katika tasnia ya burudani ya Amerika. Katika picha alizochapisha kwenye akaunti yake ya Instagram, Diamond anaonekana katika mkutano na rapa nyota wa Marekani Snoop Dogg.

Soma Pia: Wasanii 5 Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Kwenye YouTube Tanzania

Snoop Dogg ni mmoja wa wanamuziki wakongwe na wanaoheshimiwa sana duniani. Ana uzoefu mkubwa ikija kwenye masuala ya muziki na ni miongoni mwa wanamuziki waliofanikiwa zaidi ulimwenguni.

Mkutano wa Diamond na Snoop Dogg haukuwashangaza mashabiki tu bali pia ulifurahisha kumuona akiendelea kupanua mizizi yake kimuziki. Wakati wa mkutano huo, Diamond alionekana katika mazungumzo na Snoop Dogg ingawa bado haijajulikana ni nini walikuwa wakijadili. K

Katika taarifa ambayo bosi huyo wa WCB alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram, alidai kuwa ni vizuri kuchukua ushauri kutoka kwa wale ambao wamefanikiwa zaidi.

Soma Pia: Zuchu Aeleza Sababu ya Kuimba Muziki wa Singeli Kwenye ‘Nyumba Ndogo’

"Listen, learn from the kings and you will achieve more," ilisomeka taarifa ya Diamond.

Bado haijulikani iwapo Diamond atatoa wimbo na Snoop Dogg au wawili hao walikuwa wamekutana tu kwa mazungumzo. Wakati wa mkutano huo, ilifunuliwa pia kuwa mtayarishaji wa muziki wa Amerika Swizz Beats ndiye mtayarishaji mtendaji wa albamu ya Diamond.

Hapo awali Diamond pia alikuwa amekutana na nyota wengine wa Amerika kama vile Wiz Khalifa na wengine wengi. Diamond alikuwa amesafiri kwenda Marekani kuhudhuria tuzo za BET ambapo alikuwa ameteuliwa. Yeye, hata hivyo, alibaki huko kusudi aendelee kutengeneza albamu yake.

Leave your comment