Zuchu Aeleza Sababu ya Kuimba Muziki wa Singeli Kwenye ‘Nyumba Ndogo’

[Picha: Zuchu Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msani maarufu kutoka Tanzania Zuchu amefunfuka ni kwa nini aliamua kuimba mziki wa Singeli kwenye ngoma yake mpya ‘Nyumba Ndogo’. Akiongea na kituo kimoja cha habari hapa nchini Tanzania, msanii Zuchu kutokea WCB ameelezea kuwa mziki wa Singeli unapendwa sana nchini Tanzani, hivyo aliona n vyema kuwapa mashabiki wake ngoma watakayo furahia kwa mda mrefu.

Soma: Nyimbo Mpya: Lulu Diva, Lava lava Waachia Wimbo Mpya ‘Samahani’ [Video]

"Singeli ni muziki ambao naupenda sana, mi nimeudhuria matamasha na nimeshaenda club yani energy yote ikishaisha ikishafika mwisho hata watu wawe wamechoka vipi, singeli ikipigwa kila mtu anaamka, kwa hiyo, hiyo ndo inspiration yangu ilipotokea," Zuchu alieza.

Aidha kwenye mahojiano hayo, Zuchu aliweka wazi kuwa alitaka video ya wimbo huo iwe tofauti na video nyingine za singeli na alipanga kuwastaajabisha mashabiki zake kwa kufanya video ya kiutofauti.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Hamisa Mobetto Aachia Wimbo Mpya ‘Ex Wangu’ [Video]

"Hii official video watu wameipenda sana na nimepata reviews nyingi sana kuhusu hii video people are like we did not expect it. Yaani tumeifanya in a way that hata mtu wa taifa jingine akiona atasema huu ni mziki gani? Mbona video kali hivi?" alisema Zuchu.

Ikumbukwe video ya wimbo wa ‘Nyumba Ndogo’ imefanywa na muongozaji video maarufu nchini Tanzania Hanscana ambaye ukiachana na Zuchu, Hanscana ameshaongoza video za wasanii wakubwa nchini Tanzania kama Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Vanessa Mdee, Ibraah, Jux na wengineo wengi.

Siku chache zilizopita kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zuchu alizua taharuki kwa kuchapisha video iliyoonesha kuwa kuna jambo kubwa sana atalifanya ifikapo Julai 31 mwaka huu na kupitia mahojiano hayo Zuchu aliangazia kuhusiana na tangazo lake.

"Nadhani watu watakuwa wameona natease tarehe 31, kwa hiyo tarehe 12 tutaenda kujua tarehe 31 kutakuwa kuna kitu gani," alisema msanii huyo.

Leave your comment