Nyimbo Mpya: Aslay Aachia Ngoma Mpya ‘Shangingi Mtoto’

[Picha: Aslay Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Aslay ameachia ngoma mpya kwa jina ‘Shangingi Mtoto’.

‘Shangingi Mtoto’ ilitayarishwa na Swahili Beats kwenye studio ya Aslay inayojulikana kama Dingii Music. Mdundo wa wimbo huo ni wa kasi na hivyo basi kuifanya kuwa wa burudani.

Soma Pia: Wasanii 5 Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Kwenye YouTube Tanzania

Aslay anajulikana sana kwa kuimba kuhusu mapenzi, kwenye wimbo huu wa hivi karibuni, hata hivyo, anazungumza juu ya mtu ambaye ameweka vipaumbele vibaya maishani. Kwenye mistari kadhaa ya wimbo huo, Aslay anasimulia jinsi mhusika katika wimbo anauza nyumba yake ili kununua gari, na mwishowe kuuza gari kununua simu.

Soma Pia: Aslay vs Marioo: Nani Bora Zaidi katika mziki wa RnB?

"Tabia yake mtandaoni kuvimba, kwa mbwembwe ana comment kumbe gari anasisimba. Amepagawa, amepagawa. Kauza nyumba kanunua gari kaona sawa. Amepagawa, amepagawa, kauza gari kanunua simu kaona sawa," Aslay aliimba.

Wimbo wa ‘Shangingi Mtoto’ ulitolewa bila video. Inatarajiwa kwamba Aslay ataachia video ya wimbo hiyo hivi karibuni.

Wimbo huu wa ‘Shangingi Mtoto’ unakuja baada ya Aslay kuwa kimya kwa muda mrefu sana. Aslay ambaye ni miongoni mwa wanamuziki ambao walibaki na mafanikio licha ya kutengana kwa Yamoto Band, alikuwa amekaa kimya na kuwaacha mashabiki wake wakiwa na wasiwasi.

Hapo awali wadau mbali mbali kama vile mtayarishaji wa muziki Kimambo Beats walikuwa wameelezea wasiwasi wao kuhusu ukimya wa Aslay.

https://www.youtube.com/watch?v=xu1xSh63WqE

Leave your comment