Linah Akana Madai ya Kutafuta Kiki Ili Kufanikiwa Kimuziki

[Picha: Linah Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania Linah amekana madai kuwa anahitaji kiki ili kupata umaarufu zaidi katika tasnia ya muziki. Madai hayo yaliibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya sintofahamu kati ya Linah na Harmonize.

Wawili hao waliripotiwa kuwa na kutokubaliana ambayo ilimfanya Linah kuchapisha taarifa dhidi ya Harmonize. Linah hata hivyo alifuta chapisho hili kutoka kwa mtandao wa kijamii baadaye.

Soma Pia: Wasanii 5 Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Kwenye YouTube Tanzania

Katika taarifa ambayo Linah alichapisha leo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, alidai kwamba haitaji kiki ili awe maarufu. Alijitetea na kusema kuwa alifanikiwa katika tasnia ya muziki bila kiki.

Alielezea kuwa sababu ya kuchapisha taarifa yake ya hapo awali ni kwamba alihisi kuwa alikuwa amekosewa na alihitaji kuzungumza.

Soma Pia: Rosa Ree Awasihi Wasanii wa Bongo Kuacha Kufanya Kiki Katika Muziki

"Nilianza safari yangu ya mziki bila ya hizo kiki wala drama. Mashabiki wangu walinipenda mimi kupitia mziki wangu. Na pia mziki wangu huo huo umekuwa ukinitangaza bila ya hizo kiki wala drama. Ila inapofika mahali naona nakosewa heshima siwezi kukaa kimya," Linah alisema.

 Mwimbaji huyo pia alikuwa amefanya mahojiano na Clouds FM ambapo alizungumzia suala hilo. Chapisho la Linah kwenye mtandao umepokelewa kwa hisia tofauti huku mashabiki wengi wakionyesha kumuunga mkono.

Linah ni miongoni mwa wanamuziki wa Kitanzania ambao kwa sasa wanafanya vizuri na ana mashabiki wengi.

Leave your comment