Jux na Jovial Kuachia Ngoma Mpya Hivi Karibuni

[Picha: Juma Jux Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Kenya Jovial na mwanamuziki wa Bongo Juma Jux wanatarajiwa kuachia wimbo mpya hivi karibuni.

Habari za ushirikiano wao ziliibuka kwenye mtandao baada ya Jovial kuchapisha video ambayo ilimuonyesha akiwa studio na Jux.

Soma Pia: Jux Ampongeza Nikki wa Pili Baada ya Kuteuliwa Mkuu wa Wilaya

Wawili hao walionekana wakisikiliza wimbo na kuufurahia. Jovial amechapisha video kadhaa kwenye ukurasa wake wa Instagram ambazo zinamuonyesha katika kipindi kinachoonekana kuwa cha kurekodi na Jux.

Hata hivyo, Jux na Jovial hawajatangaza rasmi au kuzungumzia mradi huo wa muziki uliowaleta pamoja.

Ripoti za ushirikiano huo zinakuja muda mfupi baada ya Jovial kuachia wimbo uliopewa jina la 'Usiku Mmoja' kwa kushirikiana na mwanamuziki wa Tanzania Darassa.

Wimbo huo ambao ni mchanganyiko wa wimbo wa mapenzi na vile vile kilabu umepokelewa vizuri na mashabiki.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Jux, Jay Rox na Kenz Ville Waungana Kuachia Wimbo Mpya ‘Changanya’

Hadi sasa wimbo huo una zaidi ya watazamaji laki moja kwenye mtandao wa YouTube.

Inaonekana kwamba Jovial amekwenda kwenye misheni ya kupanua soko lake la muziki nchini Tanzania. Hata hivyo, sio Jovial tu ndio mwanamuziki wa Kenya pekee nchini Tanzania kwa sasa. Wanamuziki wengine kama Tanasha na Masauti pia wako nchini Tanzania ambapo wanatarajiwa kuwaburudisha mashabiki Jumamosi hii inayokuja kwenye tamasha la Nandy Festival.

Leave your comment