Darassa Atangaza Ujio wa ‘Loyalty’ Video Akiwashirikisha Nandy na Marioo

[Picha: YouTube]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi wa CMG Darassa ametangaza rasmi kuwa Ijumaa ya wiki hii ataachia video ya wimbo wake wa Loyalty aliomshirikisha Nandy pamoja na Marioo.

Darassa ambaye jina lake halisi ni Sharif Thabit Ramadhani ametoa taarifa hiyo kupitia akaunti yake Instagram. Darassa alichapisha video fupi kisha akaisindikiza na ujumbe : "Kuna 70% za uhakika ile video ya wimbo wako pendwa ikawa realized this Friday. Inshaallah."

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Lulu Diva, Lava lava Waachia Wimbo Mpya ‘Samahani’ [Video]

Sambamba na hilo, Darassa alitumia fursa hiyo kuwashukuru watu wote waliohusika katika maandalizi ya wimbo huo ambao ni wimbo namba tano kwenye albamu yake ya "A Slave Becomes King" iliyotoka Desemba 24 mwaka 2020.

Darassa aliendeleza ujumbe wake akiandika "Niko hapa kutanguliza shukrani zangu kwa kila ambae amejituma kufanikisha shughuli hii. Ukiacha ubora wangu wote lakini hii shughuli isingewezekana peke yangu. Asante Marioo, Nandy, The mix killer, royazdad na mokobiashara.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Video Tano za Harmonize, Diamond, Zuchu na Alikiba Zinazovuma Tanzania Wiki Hii

Kwa muda mrefu sasa wadau mbalimbali wa muziki nchini Tanzania wamekuwa wakimsihi msanii Darassa kuachia video ya wimbo huo ambao umeshashika nafasi za juu katika chati mbalimbali za muziki hapa nchini Tanzania.

Mathalani Mx Carter ambaye ni mdau mkubwa wa muziki nchini Tanzania kupitia akaunti yake ya Twitter aliona umuhimu wa wimbo huo kuwa na video, hivyo kupitia ukurasa wa Twitter Mx Carter aliandika : "Wimbo wa Darassa, Nandy & Marioo - loyalty umekosa video tu aisee… ni wimbo na Nusu…"

Kufikia sasa Darassa ameshatoa video tatu kutoka kwenye albamu yake. Video ya kwanza ilikuwa ‘I like it’ akishirikiana na Sho Madjozi iliyotoka Februari 25 mwaka 2020, ukifuatiwa na ‘Proud of You’ iliyotoka Desemba 31 mwaka 2020 kisha Februari 5 2021 akatoa video ya ‘Waiter’ ambayo imeshatazamwa takriban mara Milioni moja kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment