Baba Levo Akejeli Wasanii Wanaodaiwa Kununua Watazamaji Kwenye YouTube

[Picha: Baba Levo Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Bongo Baba Levo amejitokeza kuwadhihaki wanamuziki ambao wamedaiwa kununua watazamaji katika nyimbo zao kwenye mtandao wa YouTube.

Baba Levo wakati akiongea katika mahojiano ya hivi karibuni alieza kuwa inawezekana kununua watazamaji bandia, na kuwakejeli wasanii wanaotumia mbinu ili kuonekana ni kama kazi zinanawiri.

Soma Pia: Harmonize Ajibu Madai ya Kununua Watazamaji YouTube Kwenye Wimbo wake ‘Sandakalawe’

Baba Levo alidai kuwa kuna kampuni ambazo zinauza watazamaji bandia kwa wanamuziki na watu mashuhuri kwenye mtandao wa YouTube. Aliahidi kudhibitihsa madai hayo katika wimbo wake ujao.

Alisema kuwa atanunua watazamaji kusudi kuonyesha kuwa inawezekana kununua watazamaji. Mwimbaji huyo alimnukuu Alikiba kwa kusema kuwa kesi ya kununua watazamaji ni sawia na mtu kujitekenya ili acheke mwenyewe.

Soma Pia: Maswali Yaibuka Kuhusu Idadi ya Watazamaji Kwenye Wimbo wake Harmonize 'Sandakalawe'

"Suala la views lishajulikana kwamba kuna makampuni ambayo yanafanya kazi ya kutengeneza viewers ambayo ukilipia unatengenezewa. Mimi mwenyewe nitawaonyesha mfano katika ngoma yangu mpya nitakayoiachia. Nitalipia viewers ili waone jinsi watakavyo panda maroboti. Ni kujitekenya na kucheka mwenyewe kama alivyosema Alikiba," Baba Levo alisema.

Swala la kununua watazamaji kwenye mtandao wa YouTube limekuwa swala kubwa Bongo wiki hii, huku mashabiki wakidai kwamba msanii Harmonize alinunua views ya wimbo wake wa ‘Sandakalawe’.

Madai hayo yalitokea baada ya video ya wimbo huo kupata watazamaji zaidi ya milioni nne ndani ya siku nne.

Msani huyo hata hivyo amekana madai hayo huku akisisitiza kuwa ngoma yake inapendwa na kuskizwa sehemu mbali mbali duniani.

Leave your comment