Maswali Yaibuka Kuhusu Idadi ya Watazamaji Kwenye Wimbo wake Harmonize 'Sandakalawe'

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wimbo wa Harmonize ‘Sandakalawe’ umezua gumzo mtandaoni sababu kuu ikiwa idadi ya watazamaji iliyopata kwenye mtandao wa YouTube. Mashabiki wameibua maswali kuhusu uhalisia wa idadi ya watazamaji waliopo kwenye wimbo huo tangu uchapishaji wake.

Soma Pia: Harmonize Aeleza Kwanini Aliita Wimbo Wake ‘Sandakalawe’

Hadi sasa, video rasmi ya wimbo wa 'Sandakalawe' iliyochapishwa siku nne zilizopita, imepata takriban watazamaji milioni nne. Wadau mbali mbali katika tasnia ya muziki wamehoji idadi kubwa ya watazamaji ambao wimbo huo umepokea kwa mda mfupi.

Kwa mfano, mashabiki wengine wamedai kuwa ulinganisho baina ya idadi ya watazamaji na 'likes' kwenye wimbo huo haiendi sambamba. Cha kushangaza ni kuwa video ya 'Sandakalawe' imeshindwa kuwa namba moja kwenye orodha ya video zinazovuma kwenye YouTube licha ya kuwa na idadi kubwa ya watazamaji.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Wimbo Wake ‘Sandakalawe’

Video hiyo ilikuwa nambari nne kwenye orodha ya video zinazovuma, huku nafasi tatu za kwanza zikishikwa na Zuchu, Diamond na Alikiba mtawaliwa. Baadhi ya mashabiki wamemshutumu Harmonize kwa madai ya kununua watazamaji wa wimbo huo ili kuonekana kuwa wimbo wake ulikuwa maarufu zaidi kuliko ule wa wanamuziki wengine ambao wameachia nyimbo zao hivi karibuni.

Mashabaki walidai kuwa kuwa video hiyo ingekuwa namba moja katika orodha ya video zinazotamba zaidi iwapo watazamaji wake ni wa kweli.

Harmonize bado hajajitokeza kujibu madai ya kununua watazamaji. Ni muhimu pia kubainisha kuwa hii sio mara ya kwanza kwa Harmonize kujipata akihojiwa juu ya idadi ya watazamaji kwenye video zake mtandaoni YouTube. Video yake iliyoitwa ‘Attitude’ pia ilihusika katika madai kama haya.   Hii hapa baadhi ya maoni kutoka mtandaoni:

Leave your comment