Harmonize Aeleza Kwanini Aliita Wimbo Wake ‘Sandakalawe’

[Picha: Wikipedia]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Ukitembea mitaani, kwenye sherehe na kwenye kumbi mbalimbali za starehe wimbo wa ‘Sandakalawe’ kutoka kwa Harmonize ni mojawapo ya nyimbo ambazo zinafanya vizuri sana.

Akizungumza katika mahojiano kwenye kipindi cha Leo Tena, Harmonize alisema kuwa aliamua kuupea wimbo huo jina la ‘Sandakalawe’ kwa kuwa linawakumbusha watu michezo ya utotoni hivyo basi inafanya watu wapende kusikiliza wimbo huo.

Soma Pia: Harmonize Aeleza Kwanini Hakumtakia Heri Diamond Platnumz Kwenye BET

"Wanasemaga Old is Gold ukiwakumbusha watu zamani yaani na wao wanaenjoy lakini pia ni rahisi nyimbo kuhit mapema ukitumia maneno ya zamani," alieleza Harmonize.

Harmonize pia aligusia kwanini anapenda kuimba nyimbo za Amapiano na nyimbo zenye vionjo vya Afropop, akisema kuwa ni vyema kujarbu mbinu mpya a kutunga nyimbo ili kuwafikia watu wengi.

"Kutengeneza tu muziki wa kitanzania ni ubinafsi. South Africa ni Afrika. Nigeria ni Africa hivyo ni Culture yetu. Sio kitu kibaya kutengeneza mziki wa Bongo fleva lakini pia sio kitu kibaya kutengeneza culture ya mwenzio," Harmonize alisema.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Wimbo Wake ‘Sandakalawe’

Harmonize ambaye yuko jikoni kuivisha albamu yake ya pili tangu aanze muziki mwaka 2015 alieleza kuwa kuwa albamu yake ijayo itakuwa na aina tofauti tofauti za muziki kutokea barani Afrika.

"Kwenye albamu yangu kuna kila aina ya muziki kuna Singeli, nimefanya bongo fleva, nimefanya reggae, nimefanya Afropop, amapiano yaani kila aina ya muziki," Msanii huyo alionena.

Kwa sasa, Harmonize anatamba na wimbo wake wa Sandakalawe ambao mpaka sasa umetazamwa takriban mara 397, 000 kwenye mtandao wa YouTube.

Leave your comment