Harmonize Aeleza Kwanini Hakumtakia Heri Diamond Platnumz Kwenye BET

[Picha: The Star]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldwide Harmonize amejibu wanaouliza ni kwanini hakumtakia Diamond Platnumz heri kwenye tuzo za BET.  Harmonize akiongea na kituo kimoja cha habari nchini Tanzania alisema kuwa watu wanafaa kuheshimu maamuzi yake kwani hawafahamu nini kipo nyuma ya pazia.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Wimbo Wake ‘Sandakalawe’

"Watu waheshimu maamuzi ya watu wote ambao hawakufanya hivyo huenda mtu hakutaka au ana sababu yake binafsi. Wanasema kitanda ambacho hujakilalia huwezi kujua utamu wake ulivyo so sio kitu kibaya lakini next time inshaallah,"Harmonize alisema.

Harmonize aliongeza kwa kusema kuwa kuna kipindi hapo nyuma aliweka chapisho kumsifia msanii mwenzake lakini watu walichukulia tofauti.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aaachia Ngoma Mbili Mpya ‘Kazi Iendelee’ na ‘Tuvushe’

"Muda mwingine unaweza ukafanya jambo kwa wema tu alafu ukaonekana kama unatafuta attention," aliongeza Harmonize.

Harmonize pia alitumia fursa hiyo kueleza kwanini wasanii kama Anjella, Ibraah na Killy wanafanya vizuri ndani ya muda mfupi tu aliowasimamia. Kulingana na Harmonize, wasanii hao wamemweka Mungu mbele.

"Nadhani ni kumtegemea Mungu na kuwa positive. Ni kumtanguliza Mungu mbele na kuwa Calm ndio inasaidia."

Aidha Harmonize aliongeza kuwa iwapo msanii yoyote kutokea Konde Gang ataona kuwa yupo tayari kujisimamia mwenyewe, hatamzuia kuondoka.

Kwa sasa Harmonize anatamba na wimbo wake wa ‘Sandakalawe’ na muda wowote anaweza kutangaza ujio wa albamu yake ya pili tangu aanze muziki iitwayo ‘High School’.

Leave your comment