Nyimbo Mpya: Harmonize Aaachia Ngoma Mbili Mpya ‘Kazi Iendelee’ na ‘Tuvushe’

[Picha: The Star]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa Konde Music Worldwide Harmonize ameachia ngoma mbili mpya ‘Kazi iendelee” na ‘Tuvushe’.

Nyimbo hizi mbili ni za Kumsifu na kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Tanzania Mama Samia Suluhu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Diamond, Alikiba na Wasanii Wengine Wanoatarajiwa Kuachia Ngoma Mpya

Kwenye ‘Kazi Iendelee’, Harmonize amewashirikisha H Baba and Awilo Longomba.Ngoma hio inatumia mdundo wa wimbo wao wa ‘Attitude’.

Wimbo wa ‘Kazi Iendelee’ inamshawishi rais Suluhu na wananchi wa Tanzania kuendeleza kazi iliyoanzishwa na hayati Rais John Pombe Magufuli.

“Kazi iendelee…Tuchape kazi tusonge mbele… Kazi iendelee…Tuchape kazi tusonge mbele…,” Harmonize aliimba.

Kwenye wimbo wa ‘Tuvushe’, Harmonize anaimba kuwa Hayati Rais Magufuli alimwachia Rais Suluhu jahazi, sasa kazi yake ni kuwavusha watanzania na kuwafikisha sehemeu ile nyingine yenye maendeleo.

Soma Pia: Zuchu Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Zilizomfanya Zuchu Kuwa Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki

Harmonize anaimba kuwa Rais Suluhu ni kiongozi shupavu mwenye kupenda haki, hana fitina, na ana ndoto shupavu za wanawake.

Kwa wale wanaohofia kuwa Rais Suluhu huenda akashindwa na kazi, Harmonize anamsihi awaonyeshe jinsi anavyotekeleza miradi zilizoachwa nyuma na Rais Magufuli.

Ngoma hizo mbili zimepokelewa vyema na kwa sasa ni baadhi ya nyimbo zinazovuma nchini Tanzania.  

Harmonize sasa amejiunga na wasanii kama vile Rayvanny na Zuchu ambao wameshaachia nyimbo za kusifu na kumuunga mkono Mama Suluhu.

https://www.youtube.com/watch?v=wSm0XGVcEOQ&ab_channel=HarmonizeHarmonize

Leave your comment