Nyimbo Mpya: Harmonize Aachia Video ya Wimbo Wake ‘Sandakalawe’

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi na msanii kutokea label ya Konde Music Worldwide Harmonize ameachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Sandakalawe’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zilizoachiwa na Wasanii wa Konde Gang Mei 2021[Video]

Video hio imetengenezwa nchini Nigeria na Harmonize kwa mara nyingine ameonesha utofauti wake kwani amefanya video hiyo eneo la mtaani kabisa lakini video imependeza sana.

Ukiachana na mandhari kuwa mazuri, Harmonize amewashirkisha wacheza dansi (dancers) walioitendea haki video kwa kucheza vizuri sana.

Video ya Sandakalawe mpaka sasa imetazamwa mara ya zaidi laki moja nukta tisa kwenye mtandao wa YouTube ikiwa ni masaa machache tu tangu kuachiwa kwake

Video ya ‘Sandakalawe’ imeongozwa na Oyin Ameen mutayarishaji wa video kutokea nchini Nigeria, ambaye ameshafanya kazi na wasanii wakubwa nchini humo. Kabla ya kuwa director, Ameen alikuwa manager wa mtayarishaji muziki Kriz Beatz pamoja na rapa Ceeboi.

Ameen alianza kutengeneza video za muziki kipindi cha karantini ya Corona mwaka 2020 katika kipindi hicho alianza kusoma masuala ya filamu mtandaoni kwenye chuo cha New York Film School na tangu hapo mpaka sasa, ameshatengeneza video za muziki zaidi ya kumi na mbili.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aaachia Ngoma Mbili Mpya ‘Kazi Iendelee’ na ‘Tuvushe’

Bado haijawekwa wazi kama wimbo huu wa ‘Sandakalawe’ utakuwepo pia kwenye albamu inayofuatia ya Harmonize, lakini mpaka sasa wimbo huu ni wimbo wa tatu wa Harmonize tangu mwezi Juni uanze, nyingine zikiwa ni ‘Tuvushe’ pamoja na ‘Kazi iendelee’ zilizotoka Juni 12 mwaka huu.

https://www.youtube.com/watch?v=JWDTQdQgd4o

Leave your comment