Romy Jones Aeleza Faida za Mitandao ya Kuuza Muziki Tanzania

[Picha: Mpasho]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

DJ Romy Jones ambaye pia ni naibu rais wa lebo ya rekodi ya WCB amepongeza uwepo wa mitandao za kuuza muziki. Romy Jones ambaye alikuwa akizungumza wakati wa mahojiano ya hivi karibuni alisema kwamba mitandao kama hizo zimesaidia tasnia ya muziki kukua kwa kasi sana.

Soma Pia: Romy Jones Aapa Kuwasaidia Wasanii Wachanga Kujiendeleza Kimuziki

Romy Jones alielezea hali ya muziki kama taaluma sasa ilikuwa bora na faida zaidi ikilinganishwa na hapo awali ambapo mitandao za kuuza miziki hazikuwepo.

Alisema kuwa wanamuziki sasa wanaweza kupata pesa kutoka kwa ngoma zao na kuiwekeza kipato hicho kwenye muziki. Alifafanua pia kuwa mapato ya wanamuziki hutofautiana kulingana na mambo anuwai. Kulingana na Romy Jones, wanamuziki tofauti wana mikakati yao ambayo itawafanya wakue na kupata kipato zaidi.

Soma Pia: Romy Jones Azungumzia Wanaomkashifu Diamond Kwa Kuteuliwa Kwenya Tuzo za BET

"Sasa hivi inasaidia kidogo, Alhamdulilahi tunapata pesa ambayo sio nyingi. Huwezi kusema inarudisha kwenye album au inarudisha kwenye nyimbo ambayo ume invest au kwenye video, lakini kwa namna moja au nyingine unaona kwamba kabisa nikiendelea kufanya nitapata kikubwa zaidi. Japo wao wanaopata kikubwa ambao wana content nyingi," Romy Jones alisema.

Aidha Romy Jones aliahidi kutoa nyimbo kadhaa baadaye mwaka huu. Wanamuziki wa Tanzania wamekuwa mstari wa mbele kujenga uwepo wao kwenye majukwaa anuwai ambayo yanauza muziki.

Hivi karibuni Harmonize aliasaini mkataba na jukwaa jipya ambalo litawawezesha mashabiki wake kulipa ili kutazama matamasha yake kwenye mtandao.

Leave your comment