Romy Jones Aapa Kuwasaidia Wasanii Wachanga Kujiendeleza Kimuziki

[Picha: Romy Jones Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Naibu rais wa WCB Romy Jones ambaye pia ni kaka wa Diamond Platnumz ameapa kuwaunga mkono wanamuziki wachanga. Akiongea wakati wa mahojiano ya hivi karibuni, Romy Jones alisema kwamba anataka kuwa mtu ambaye atawaunganisha wanamuziki mashuhuri na wale ambao bado ni wachanga kimziki.

Soma Pia: Babu Tale Amsifu Nandy Baada ya Tamasha Yake ‘Nandy Festival’ Kufanya Vyema

Romy Jones alielezea kuwa ana shauku kubwa ya kusaidia wanamuziki wachanga wenye talanta kujenga taaluma zao katika tasnia ya muziki wa Tanzania. Alifunua kuwa ni ndoto yake kuunganisha wanamuziki kutoka pande tofauti za ulimwengu na kuwaleta kushirikiana kwenye miradi za muziki.

Alitoa mfano wa jinsi angependa kuleta Marioo wa Tanzania kufanya kazi na Sho Madjozi kutoka Afrika Kusini, na pia kuwaleta pamoja Rayvanny na Meddy wa Rwanda.

Soma Pia: Weusi Waeleza Jinsi Kundi Lao Litabadilika Baada ya Nikki wa Pili Kufanywa Mkuu wa Wilaya

"Nimeamua kukuwa kama connector, mtu ambaye nipo katikati, middle man. Yaani ukitaka Chichi unachukua unaleta kwangu napeleka huku and I am doing that for love, Nafanya kwa mapenzi sifanyi kwa kulipwa. Ndio maan niko hapa kama DJ ambaye ntamchukua Rayvanny, ntamchukua na Meddy from Rwanda ntawaeka pamoja watatoa kitu kimoja. Nitamchukua Marioo nitamchukua Sho Madjozi from South Africa na watafanya kitu kimoja. Hio ndio target yangu kusaidia watu wote," Romy Jones alieleza.

Romy Jones ambaye ni DJ rasmi wa WCB amesifiwa na wanamuziki wengi wachanga kwa kuwaunga mkono na kusimama nao.

Leave your comment