S2kizzy Azungumzia Ujio wa Albamu Mpya ya Diamond Platnumz

[Picha: S2kizzy Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji muziki kutokea nchini Tanzania Salmin Kasimu Maengo almaarufu kama S2kizzy ameelezea kwa undani hali ilivyo kufanya kazi na Diamond PLatnumz kwenye albamu yake mpya inayotarajiwa kuachiwa hivi karibuni.

Soma Pia: Romy Jones Aapa Kuwasaidia Wasanii Wachanga Kujiendeleza Kimuziki

Akiongea na chombo kimoja cha habari hapa nchini Tanzania, S2kizzy ambaye kashafanya kazi nyingi na Diamond Platnumz kama "Kanyaga", "Far away" pamoja na "Baba Lao" ameelezea kuwa anafurahia kuhusishwa kwenye utayarishwaji wa albamu ya Diamond na ni heshima kubwa sana amepewa kushiriki kwenye maandalizi ya albamu hiyo.

"Ilikuwa tu ni moja kati ya kitu ambacho nasema ni appreciation, pia kama mtu kaona uwezo wako its all about ufanisi wako kujituma creativity yeah thats all," S2kizzy alisema.

Soma Pia: AT Azungumzia Uhasama wa Jadi Baina ya Diamond na Alikiba

Producer huyo pia aligusia mambo aliyojifunza baada ya kusafiri na Diamond Platnumz kuelekea Afrika Kusini kuandaa albamu hiyo mwezi Aprili. "Naeza, nikasema nimepata experience kubwa coz you know ye Diamond tayari ni msanii mkubwa. Nimepata experience ya kitofauti, knowledge tofauti, management tofauti, watu wako serious kwenye muziki," S2kizzy alinena.

"Pia nimejifunza businesswise katika music its not only about entertainment, sometimes its all about business so inabidi ujue hivi vitu viwili kuentertain at the same time uwe katika business way," alifunguka S2kizzy.

Kwenye mahojiano hayo pia, S2kizzy aligusia sakata la Diamond Platnumz kusemekana kutumia vionjo vya wimbo wa ‘Essence’ kutokea kwa msanii Wizkid wa Nigeria, ambapo mtayarishaji huyu amewasihi mashabiki kuacha kufikiri kuwa kuna ugomvi baina ya wasanii hao wakubwa barani Afrika kwani Diamond na Wizkid ni marafiki wazuri tu.

"Diamond na Wizkid ni washikaji so wana kazi zipo washafanya na sio moja so wanaongea, kwa hiyo watu wakawa wanaweza wakawa wanaona hivi kumbe ni hivi, kwa hiyo its all good. Nadhani angekuwa mtu hajapenda asingeandika kitu," producer huyo alisema.

Leave your comment