AT Azungumzia Uhasama wa Jadi Baina ya Diamond na Alikiba

[Picha: The Citizen]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania AT amefunguka kuhusu uhasama wa muda mrefu kati ya wanamuziki Diamond Platnumz na Alikiba. Wanamuziki hao wawili ni miongoni mwa wapinzani wakongwe katika tasnia ya burudani ya Tanzania.

Ushindani wao ulianza muda mrefu uliopita wakati AT alikuwa bado anatamba sana kwenye tasnia ya muziki kabla ya kudidimia na kuenda kimya.

Soma Pia: Anjella Amshirikisha AT "Si Saizi Yako’: Nyimbo Mpya Tanzania [Official Audio]

Wakati huo, AT alikuwa maarufu sana na wakati mmoja alikosolewa vikali sababu kuu ikiwa maoni yake kuhusu ushindani wa Alikiba na Diamond Platnumz.

Mwimbaji huyo sasa amefunguka na kubaini kuwa alitukanwa kwa kile alichosema. Katika mahojiano ya hivi karibuni, AT alijitetea akisema kwamba hakuwa na nia mbaya dhidi ya Diamond au Alikiba.

Soma Pia: Harmonize Aanzisha Safari ya Kuinua Mziki wa Zanzibar Kupitia Wimbo Mpya wa Anjella

Alifafanua kuwa hatachukua upande wowote katika ushindani huo kwa sababu Alikiba na Diamond walikuwa marafiki wake wa zamani.

Aliongeza, hata hivyo, kuwa atakosoa kila mmoja wao wakati wowote wanapofanya jambo baya. AT aliendelea na kufichua kuwa aliwahi kumwendea Alikiba na kumshauri asizingatie uhasama huo kwa kina. Alimwambia Alikiba kuwa ushindani kama huo unaweza kuwa na athari mbaya kwenye kazi yake ya muziki.

"Haikuwa na ubaya ati kwa kuwa namuattack mtu mwengine. So nimekaa kwenye uhalisia. Mimi simpendelei mtu, kama kuna mahali naona labda ata Ali alikuja kukosea nasema," AT alieleza.

Leave your comment