Anjella Amshirikisha AT "Si Saizi Yako’: Nyimbo Mpya Tanzania [Official Audio]

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa Konde Gang Anjella ameachia wimbo mpya alioshirikiana na msanii gwiji wa mziki wa mduara kutoka Zanzibar  kwa wimbo “Si saizi yako”.

Katika wimbo huu wawili hao wanaonya  mahasidi wao ya kuwa wao hawaafikiani kimaisha. AT anaanza wimbo  huu kwa ujuzi mkubwa kwa kukosoa hulka za wanaojaribu kujipendekeza kama gwiji ila hajui lolote.

“Utamaliza Mafusho mwenzetu kujifukiza ujitoe jasho kama vile wafukuzwa, Na nikupe taarifa , mjini watu tunapeta, tena ninawajibika kula yangu hakika…” aliimba AT.

Soma Pia: Zuchu ‘Nyumba Ndogo’: New Music Tanzania [Official Dance Video]

Kwa upande wake Anjella aliingia kwenye kifungu chake kwa sauti nzuri akisistiza kwa nini yeye “Si Saizi Yako”. Wimbo ulifanyiwa maandalizi na Producer Tegi.

Wimbo huu umepokelewa vizuri huku kanda yake ikitarajiwa hivi karibuni. Kwa sasa ina watazamaji zaidi ya elfu hamsini na Tano kwenye YouTube muda mfupi baada  ya kuachiwa.

Hii ni kazi yake  AT ya kwanza  baada ya muda mrefu wa Ukimya. AT anajulikana kwa kazi zake nzuri za mziki wa Mduara miaka michache iliyopita. Mduara ni moja ya fani ya mziki kutoka Tanzania uliofana sana na wasanii wengi wa mziki huu walitoka Zanzibar.
 Ila baaada ya mziki wa Bongo fleva ya kizazi kipya ilivyochukua usukani wa mziki wasanii wa mduara walianza kusahaulika.
Hata hivyo wimbo huu wa “Si Saizi yako “ unampa AT fursa ya kuirejesha fani ya mziki wa Mduara kwenye ulingo mkuu wa sanaa nchini Tanzania na bara la Afrika Mashariki. Vile vile AT anatarajiwa kushirikishwa kwenye albamu mpya ya Harmonize itakayoachiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=40M5A0_RFNs&ab_channel=AnjellaAnjella

 

Leave your comment