AT Afichua Upinzani Alioupata Baada ya Kufanya Kazi na Konde Music Worldwide

[Picha: Bongo 5]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki wa Tanzania AT amebaini kuwa alikumbana na upinzani kutokana na wimbo wake wa hivi karibuni ambao aliutayarisha kwa kushirikiana na Anjella kutoka Konde Worldwide Music.

Ushirikiano huo uliwezeshwa na Harmonize ambaye anamiliki lebo hiyo ya kurekodi muziki. Hapo awali, Harmonize alikuwa ameapa kuinua kiwango cha muziki kutoka Zanzibar. Anaonekana kuanza kutekeleza ahadi hiyo kwa kumkaribisha AT kwenye Konde Worldwide Music.

Soma Pia: Sina Chuki na Diamond- AT Aeleza ya Kufanya Kazi na Konde Worldwide

Alipokuwa akiongea wakati wa mahojiano ya hivi karibuni na mwandishi wa habari Skywalker, AT alifichua kuwa kuna wale ambao walikuwa wakimtarajia arithi uhasama wa Harmonize na Diamond Platnumz.

Mwimbaji huyo, hata hivyo, alisema kwamba hatazingatia uhasama ambao Harmonize na Diamond wanao, lakini badala yake atafanya kazi ya kutengeneza muziki mzuri.

Kulingana na AT, watu wana maoni mabaya kwake Harmonize. Alielezea kuwa Harmonize hana wakati wa mashindano na ni mtu ambaye anazingatia maendeleo kila wakati. AT alifafanua kuwa baada ya kutangamana na Harmonize kwa muda mfupi, alikuwa amekuja kujifunza kuwa Harmonize ni tofauti sana na jinsi watu wanavyofikiria.

Soma Pia: AT Azungumzia Uhasama wa Jadi Baina ya Diamond na Alikiba

Kwa hivyo alitangaza kuwa atapuuza uvumi uliopo mtandaoni badala yake kuzigatia kazi.

"Wako watu hawakupenda, kwa sababu nina Harmonize. Wanataka mimi ni matatizo yako ambayo ni watu wengine wa kibiashara. Laikini mimi siwezi kufanya kazi, kuwatumikia watanzania, kwa sababu naamini hivyo hivyo vinahitaji watu wakipeleka mbele," AT alieleza.

Leave your comment