Nyimbo Mpya: Menina Aachia ‘Nyumba Kubwa’ Baada ya Zuchu Kutoa ‘Nyumba Ndogo’

[Picha: Menina Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Muigizaji maarufu wa Tanzania Menina amezua hisia tofauti baada ya kuachia wimbo mpya kwa jina ‘Nyumba Kubwa’.

Wimbo huo unakuja muda mfupi baada ya Zuchu kuachia wimbo wake ‘Nyumba Ndogo’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya : Zuchu Aachia ‘Nyumba Ndogo’, Ngoma Mpya ya Singeli

Wimbo wake Menina umeonekana kuwa na uhusiano wa karibu na nyimbo ambayo Zuchu aliachia hivi karibuni. Maudhui katika wimbo wa ‘Nyumba Ndogo’ ya Zuchu ni uke wenza. Zuchu katika wimbo wake amechukua uhusika wa mke mdogo, au ukipenda mke wa pili. Menina pia katika wimbo wake amechukua mada hiyo ya uke wenza , lakini amebadilisha uhusika na kuchukua nafasi ya mke mkubwa.

Nyimbo hizi mbili zinaangazia mada ya uhusiano kati ya wake-wenza. Zuchu hivi karibuni alitoa maoni yake kwenye chapisho ambalo Menina aliweka mtandaoni.

Soma Pia: Naibu Rais wa WCB Rommy Jones Amuagiza Diamond Kuachia Wimbo Mpya

Menina kwenye chapisho hilo alikua anatambulisha kazi yake mpya ya 'Nyumba Kubwa'. Katika maoni yake, Zuchu alicheka na kuwaacha mashabiki na maswali mengi.

Wimbo wa Menina ‘Nyumba Kubwa’ umepokelewa vyema na mashabiki na unafanya vizuri sana kwenye mtandao wa YouTube.

Kwengineko, video ya densi ya ‘Nyumba Ndogo’ ndio ngoma inayotamba zaidi YouTube Tanzania wiki hii. Video hio ilioachiwa siku chache iliyopita imetazamwa zaidi ya mara milioni moja nukta sita.

https://www.youtube.com/watch?v=M0a7ooFLAWw

Leave your comment