Nandy Aeleza Sababu ya Kuandika Wimbo wake Mpya ‘New Couple’

[Picha: Nandy Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki iliyopita, Nandy aliachia EP yake ya pili mwaka huu iitwayo Taste. EP hiyo iliyotengenezwa na watayarishaji wakubwa wa muziki hapa nchini Tanzania kama vile Mr LG, T Touch na Kimambo ina jumla ya nyimbo nne mojawapo ikiwa ni "New Couple" .

Kwenye wimbo huo wa ‘New Couple’,  Nandy ameongelea namna ambavyo mahusiano ya watu maarufu hayadumu na pia ndani ya wimbo huo ametaja watu maarufu tofauti tofauti ambao wameshawahi kuachana na wenzi wao kama vile Vanessa, Jux, Esma, Harmonize, Aunty Ezekiel, Kajala, Queen Darleen na Petty man.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Nandy Azungumzia Mahusiano ya Rayvanny, Harmonize na Jux Kwenye ‘New Couple’

Baada ya kumaliza tamasha lake la Nandy Festival huko Mwanza, Nandy alipata wasaa wa kuongea na wanahabari na akaeleza kwanini aliimba wimbo huo ambao mpaka sasa hauna video.

"Ni couple ambazo nilikuwa nazipenda na pia hata huko walipohamia pia napapenda. Popote walipo nipo kwa hiyo niliimba tu kwa feeling na idea ambavyo ilikuja," Nandy alisema.

Nandy aliongezea kuwa baada ya kuwaimba mastaa hao kwenye wimbo wake huo, hakuna hata mmoja aliyechukia au kumkemea kwa yeye kuwataja.

Soma Pia: Nandy Asafiri Nigeria, Atarajiwa Kuachia Kazi Mpya na Wasanii Wakubwa Naija

"Wanaelewa sio mara yao ya kwanza wao kuimbwa , wanaimbwa sana majina yao yanatajwa sana,” Nandy alidokeza.

Kando na hilo, msanii Nandy pia amesema kwamba wiki ijayo ataachia video ya ‘Nimekuzoea’ hivyo mashabiki zake wakae mkao wa kula. Tangu aanze muziki rasmi mwaka 2016 mpaka sasa, Nandy ameshaachia albamu moja inayoitwa African Princess na mwaka 2021 mwezi Machi aliachia EP iliyosheheni nyimbo za dini tu iitwayo ‘Wanibariki’.

https://www.youtube.com/watch?v=1veAMqS2VpY

Leave your comment