Harmonize Afunguka Kuhusu Uteuzi wa Diamond Kwenye BET

[Picha: Harmonize Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mkurugenzi mkuu wa Konde Gang Harmonize amezungmzia tetesi zilizoikumba uteuzi wa Diamond kwenye tuzo za BET, na kusema kwamba kila mtu ana haki ya kusema kile anachatoka kuhusu jambo hilo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wake na kampuni ya Ceek, Harmonize alidai kwamba anaheshimu maoni ya watu. Alielezea kuwa watu wana haki ya kutoa maoni yao kwa uhuru, iwe ni kumuunga mkono Diamond au kumkosoa. Hata hivyo, Harmonize alikataa kusema wazi iwapo anaunga mkono au haungi mkono uteuzi wa Diamond.

Soma Pia: Anjella Amshirikisha AT "Si Saizi Yako’: Nyimbo Mpya Tanzania [Official Audio]

"Mimi nadhani, kama nilivyosema mwanzo kwamba kila mtu ana mtazamo wake kila mtu anafanya maamuzi yake. Wakati huo watu wakisema wamo, kuna engine walipiga kampeni kwamba ashinde, kwa hivyo kugundua kwamba kila mtu ana mtazamo wake, kwa hivyo haustahili kumwona mtu kwa mtazamo amka," Harmonize alisema.

Hapo awali, kikundi cha watanzania walianzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii ili Diamond aondolewe kutoka tuzo za BET.  

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Harmonize Aaachia Ngoma Mbili Mpya ‘Kazi Iendelee’ na ‘Tuvushe’

Kulingana na kikundi hiki, Diamond hastahili uteuzi huo kwa kuwa aliunga mkono serikali ya hayati rais John Pombe Magufuli ambayo imeshutumiwa kwa madai ya kutozingatia demokrasia na haki za wananchi, hasa katika kua zilizofanyika mapema mwakani.

Kampeni hiyo hata hivyo haikufanikiwa.

Leave your comment