Video ya Diamond Platnumz Kwenye Instagram Yazua Gumzo Mtandaoni

[Picha: Diamond Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Bosi na mwanamuziki kutokea lebo ya WCB Diamond Platnumz amezua gumzo mtandaoni, baada ya kuchapisha video fupi kupitia akaunti yake Instagram ikimuonesha akiimba wimbo inayokisiwa kuwa ngoma yake itakayotoka hivi karibuni.

Soma Pia: Soma Pia: Lava Lava ft Mbosso 'Basi Tu': Nyimbo Mpya Tanzania [Video]

Video hiyo fupi yenye urefu wa takribani dakika moja ilichapishwa muda wa 00:38 usiku na ndani ya saa moja tu, ilitazamwa takriban mara 96,000 huku blogi tofauti tofauti za kitanzania zikiripoti kuwa huenda Diamond amechapisha video hiyo ili kuwaandaa mashabiki juu ya ujio wake mpya.

Kando na Diamond kurekodi video hiyo akiwa kwenye gari lake mpya, kitu kingine kilichozua gumzo ni mrembo aliyekuwa na Diamond kwenye video hiyo ambaye bado watu wengi hawamfahamu.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Diamond, Alikiba na Wasanii Wengine Wanoatarajiwa Kuachia Ngoma Mpya

Mara tu baada ya kuchapisha video hiyo watu wengi maarufu ndani na nje ya Tanzania kama Salama Jabir, Rayvanny, Baba Levo, Gigy money, S2kizzy, Rommy Jones, Uncle Shamte pamoja na msanii kutokea Zimbabwe King 98 walitoa maoni yao wakionesha kufurahia video hiyo.

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Diamond platnumz kuachia wimbo ilikuwa ni November 30 mwaka jana alipotoa wimbo wake wa Waah aliyomshirikisha Koffi Olomide kutokea Congo. Video ya Waah imeshatazamwa takriban mara milioni 70 ndani ya siku 187 tangu kuchapishwa kwake kwenye account yake ya YouTube.

"Sina haraka ya kutoa nyimbo. Ndio maana mwaka jana nlitoa nyimbo mbili na mauzo yake na rekodi zake zikakua kubwa. Mwaka huu hadi leo sijatoa wimbo,". Diamond alieleza kwenye mahojiano na kipindi cha Refresh baada ya kuulizwa kwanini hajatoa wimbo mpaka sasa.

Swali wanalojiuliza mashabiki wengi wa Diamond Platnumz ni lini msanii huyo ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa Zoom Extra, Wasafi Records na Wasafi Media atatoa wimbo mpya.

Itazame Video Hio HAPA

Leave your comment