Diamond Azungumzia Kupigwa Vita Baada ya Uteuzi wake kwenye Tuzo za BET

[Picha: Grammy]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mwanamuziki nyota wa Tanzania Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya lawama dhidi yake kutokana na uteuzi wake kwenye Tuzo za BET.

Soma Pia: Nyimbo Mpya : Zuchu Aachia ‘Nyumba Ndogo’, Ngoma Mpya ya Singeli

Akizungumza wakati wa mahojiano ya hivi karibuni, Diamond alisema kwamba anaheshimu maoni ya kila mtu. Alielezea kuwa hawalaumu wakosoaji wake kwa msimamo wao akisema kuwa wana sababu yao ya kumkosoa.

"Mimi naheshimu mawazo ya kila mtu. Mtu akinifurahia, akinichibua, mini naheshimu,” alisema Diamond.

Wakosoaji wa Diamond walidai kuwa msanii huyo aliunga mkono serikali ya rais wa zamani wa Tanzania John Magufuli Pombe. Walibaini kuwa Diamond hajawahi kusimama kwa haki na hakustahili uteuzi wa BET.

Soma Pia: Diamond Platnumz Atangaza Kuachia Wimbo Mpya Hivi Karibuni

Wakosoaje wake walianzisha kampeni mtandaoni kuwasihi BET kumtupa Diamond nje ya tuzo hizo za kifahari.

Diamond Platnumz ni miongoni mwa wanamuziki watatu wa Afrika ambao waliteuliwa katika kitengo cha Best International Act.

Wanamuziki wengine wa Kiafrika ambao pia waliorodheshwa katika kitengo hicho ni pamoja na Wizkid na Burna Boy.

Kwengineko, Diamond ametangaza kuwa atakuwa akiachia ngoma mpya hivi karibuni, baada ya kukaa miezi sita bila kuachia ngoma ya kipekee.

Wimbo wake wa mwisho ulikuwa ‘Waah’ aliyomshirikisha msanii gwiji kutoka Congo Kofi Olomide.

Leave your comment