Producer Kimambo Beats Azungumzia Ukimya wa Aslay

[Picha: Kimambo Beats Instagram]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania Kimambo Beats amejitokeza kutoa maoni yake juu ya ukimya wa Aslay kwa muda mrefu.

Kimambo Beats ambaye aliwahi kufanya kazi na Aslay amesema sio kawaida kwa mwanamuziki hodari kama Aslay kutoweka kwa muda mrefu.

Soma Pia: Aslay vs Marioo: Nani Bora Zaidi katika mziki wa RnB?

Alidokeza kuwa alikuwa gizani pia kuhusu mahali alipo Aslay, na kuongezea kuwa alikuwa mmoja wa wanamuziki bora ambaye amewahi kufanya kazi naye.

Kimambo Beats ameongeza kuwa Aslay ana timu nzuri ya utengenezaji na kwa hivyo haipaswi kuwa shida kutoa nyimbo.

Soma Pia: Kimambo Beats Ajibu Madai Kuwa Midundo Zake Zinafanana

“Mimi nadhani kwa sasa hivi Aslay ni mtu ambaye ana production nzuri. Hilo ni jambo moja nataka ufahamu kwa sababu nikiskiliza ngoma zake naona hizi ngoma ni hatari," Kimambo Beats alisema.

Kimambo Beats alibainisha kuwa pengine suala hilo linaweza kuwa kwa wawekezaji wa Aslay, akitoa mfano kwamba wawekezaji wengi sasa wanataka kuweka pesa zao katika miradi yenye faida.

Ni muda mrefu tangu Aslay atoe wimbo na anaonekana kutofanya kazi katika tasnia ya burudani kama ilivyokua hapo nyuma. Miaka kadhaa iliyopita, Aslay alikuwa mmoja wa wasanii mashuhuri katika tasnia ya muziki wa Tanzania. Alikuwa wakati mmoja akilinganishwa na bosi wa WCB Diamond Platnumz.

Leave your comment