Kimambo Beats Ajibu Madai Kuwa Midundo Zake Zinafanana

[Picha: Kimambo Touches Facebook]

Mwandishi: Brian Sikulu

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania Kimambo Beats amejitokeza kujibu madai kwamba midundo zake zinafanana kila wakati. Akizungumza wakati wa mahojiano ya hivi karibuni, Kimambo Beats alipuuzilia mbali ripoti hizo akisema kuwa hazina msingi.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Aslay Aachia Wimbo Mpya 'Vumilia'

Aliongeza zaidi kuwa watu wanaotoa madai hayo hawaelewi kazi yake vizuri. Kulingana na Kimambo, hajawahi kurudia midundo yake na hubadilika kila wakati akifanya kazi na wanamuziki tofauti.

Alitoa mfano wa wanamuziki ambao amefanya nao kazi na jinsi midundo ilikuwa tofauti na kila mmoja.

Miongoni mwa wanamuziki bora ambao mtayarishaji wa muziki huyo amefanya kazi nao ni Nandy, Jux, S2kizy, Shetta kati ya wengine.

Soma Pia: Aslay vs Marioo: Nani Bora Zaidi katika mziki wa RnB?

Kimambo Beats, hata hivyo, alifafanua kwamba baadhi ya mashabiki wake wanaweza kukosea na mradi ambao aliulifanya zamani. Katika mradi huo, Kimambo Beats alitengeneza mdundo mmoja na kuwapa wasanii tofauti kuimba wakitumia.

"Audience mashaidi, toka nipige Papa ya Gigy Money sijawahi kurudia. Toka nipige banana ya Dogo Janja sijawahi kurudia. Toka nipige nyimbo zangu zote almost ambazo zimefanya vizuri sijawahi kurudia style," Kimambo alisema.

Kimambo pia alifunua kuwa hivi karibuni atazindua mradi wa muziki ambao amekuwa akiufanyia kazi kwa muda mrefu sana.

Leave your comment