Lava Lava ft Mbosso 'Basi Tu': Nyimbo Mpya Tanzania [Video]

[Picha: The Standard]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika kutoka Tanzania Lava Lava ameachia video ya wimbo wake ‘Basi Tu’ akimshirika Mbosso.

‘Basi Tu’ ni mojawapo ya ngoma kutoka kwenye EP yake Lava Lava kwa jina ‘Promise’.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Diamond, Alikiba na Wasanii Wengine Wanoatarajiwa Kuachia Ngoma Mpya

Kwenye wimbo huu, Lava Lava anaeleza jinsi mpenzi wake anamuonyesha dharau na kumringia ilhalli hajui shida iko wapi.

Lava Lava anaeleza kuwa anampenda mpenzi wake na haelewi ni kwa nini anamfanyia mambo hayo ya uchungu.

“Siku hizi hanipigii Hata akikuta missed call zangu Simu hashiki na akishika Anauliza nani mwezangu Mara anakata Mara simu hewani haongei Namaliza vocha Anajizima data eti amepanda bei Kunifanya ndodocha… Anajua nampenda (Basi tu)… Anafanya kusudi kuniumiza (Basi tu)
Ili mradi kuniliza (Basi tu)… Anafanya kusudi kuniumiza (Basi tu)… Ili mradi kuniliza… Aah ...aah ...aah,” Lava Lava aliimba.

Soma Pia: Wimbo ‘Sere’ wa Zuchu na Ola Kira Wafikisha Watazamaji Milioni Mbili

Video ya ngoma hii imetengezwa kwa ustadi na inaonyesha shida wanazopitia Lava Lava na Mbosso wanapojaribu kumshawishi msichana huyo kubadili mienendo zake.

Video hii imepokelwa vizuri na kwa sasa inawatazamaj zaidi ya lakini moja massa kadhaa baada ya kuachiliwa.

Video hiyo ni mojawapo ya kazi zilizoachiwa na lebo ya wasafi mwezi huu wa Juni 2021. Mapema wiki hii, Mbosso aliachia video ya ngoma yake kwa jina ‘Mseleleka’ akimshirikisha Baba levo.

https://www.youtube.com/watch?v=_Lr3MmxWgJ0

Bible Verses I DJ Mix 2021 I Football Predictions For Today I   Davido Latest Songs I Diamond Platnumz

Leave your comment