Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Mpya Zinazovuma Bongo Juni 2021

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii wa Bongo Fleva wanaendelea kuonyesha umahiri wao eneo la Afrika Mashariki kwakuachia ngoma mpya zinazotamba.

Wiki hii, wasanii kadhaa wameachia nyimbo mpya. Katika nakala hii, tunaangazia ngoma zinazotambaa kwenye mtandao wa YouTube Tanzania:

Soma Pia:Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Kali Zilizoachiwa na Wasanii wa Konde Gang Mei 2021[Video]

Cheketua – Barnaba Classic ft Alikiba

Msanii nguli wa mziki wa Bongo Barnaba aliachia wimbo mpya ‘Cheketua’ akimshirikisha mkurugenzi mkuu wa Kings Music Alikiba.

Huu ni wimbo wenye maudhui ya upendo.

 “…Nikupe habari tangu nirudi safari nikakupata kimwali tumeshinda dhohari nitazungumza nae bibi na babu wataridhia siku ya ndoa shela wigi mie kanzu na jambia tumeshinda vizingiti wambea hamtutishi…” aliimba Barnaba.

Kwa sasa, huu ndio wimbo unaotamba zaidi Bongo na unawatazamaji zaidi ya milioni moja nukta mbili.

Soma Pia: Nyimbo Mpya Zilizoachiwa na Zuchu, Rayvanny, Mbosso na Lava Lava Mwezi Mei 2021 [Video]

https://www.youtube.com/watch?v=VBEgi1Bl4Ws

Do Lemi Go - MC Kinata ft Ibraah

Huu ni wimbo wa Singeli wake MC Kinata ambao alimshikisha Ibrah kutoka Konde Music Worldwide. Kwenye mistari yao Kinata, anaimba kuhusu upendo huku Ibraah akitupa michambo. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya laki tano kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=VubqA0ej12w

Rostam ft Ferooz - Hujambo Mwanangu

Kwenye wimbo huu, Rostam wamemshirikisha msanii mwenzao maarufu Ferooz. Katika mistari yao, wanaangazia kazi aliyofanya hayati rais John Pombe Magufuli na rais wa sasa Samia Suluhu. Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya laki saba.

https://www.youtube.com/watch?v=Ql4wkqmqyQ8

Roho – Killy

Huu ni wimbo wa kwanza wa msanii Killy tnagu ajiunge na lebo ya Konde Music Worldwide. Kwenye wimbo huu, amakashifu mpenzi wake kwa kuondoka bila kumuarifu. ‘Roho’ imepokelewa vizuri na inawatazamaji zaidi ya laki moja masaa chache baada ya kuachiwa.

https://www.youtube.com/watch?v=ZA-xQAvmsTw

Mapenzi – Rich Mavoko

Orodha hii ianakamilishwa na wimbo wake Rich Mavoko kwa jina ‘Mapenzi’. Kwa jina inavyoashiria, ngoma hii ni yenye maudhui ya mapenzi. Kwa sasa, inawatazamaji zaidi ya milioni moja nukta moja.

https://www.youtube.com/watch?v=1Ralqya7aRQ

Leave your comment