Nyimbo Mpya: Barnaba Classic, Alikiba Waachia Wimbo Mpya ‘Cheketua’

[Picha: Alikiba Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii nguli wa mziki wa Bongo Barnaba ameachia wimbo mpya ‘Cheketua’ akimshirikisha mkurugenzi mkuu wa Kings Music Alikiba.

Wawili hao wameachia wimbo huu wenye maudhui ya upendo na Barnaba anaanza kwa kumumiminia mpenzi wake sifa za upendo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Mpya Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

Aliimba jinsi walivyoptana na kulezea kuwa yuko tayari kufunga ndoa nae. Vile vile, anawaonya wenye chuki na wambea kuwa mapenzi yao ni ya kudumu milele.

 “…Nikupe habari tangu nirudi safari nikakupata kimwali tumeshinda dhohari nitazungumza nae bibi na babu wataridhia siku ya ndoa shela wigi mie kanzu na jambia tumeshinda vizingiti wambea hamtutishi…” aliimba Barnaba.

Soma Pia: Tamasha la Siku ya Afrika: Zuchu Atumbuiza Mashabiki na Ngoma Zake Sukari, Cheche [Video]

Kwa upande wake, Alikiba anaombea ahadi za maisha marefu kati ya wanandoa hao.

Mdundo wa ‘Cheketua’ ni wa kipole na mtindo wake ni ule wa harusi. Wakati mashabiki wanaendelea kuupokea wimbo huu, ni dhahiri kuwa Barnaba Classic na Alikiba ni magwiji kwenye sanaa yao.

Kufikia sasa, wawili hao wamezua guzmo kuhusu ‘Ndoa’ ya Barnaba Classic ambayo kwa sasa dhamira yake kuu bado haijulikani.

Kwenye mtandao wa YouTube, wimbo huu unaendelea kupata umaarufu na watazamaji zaidi ya elfu thelathini na nane kwa sasa.

Kanda ya wimbo huu inatarajiwa hivi karibuni.

https://www.youtube.com/watch?v=iAXPKZsVhL4

Leave your comment