Nyimbo Mpya: Ngoma 5 Mpya Zinazovuma Bongo Wiki Hii [Video]

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Omondi Otieno

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wasanii wa Bongo Fleva wanaendelea kuonyesha umahiri wao eneo la Afrika Mashariki kwakuachia ngoma mpya zinazotamba.

Wiki hii, wasanii kadhaa wameachia nyimbo mpya. Katika nakala hii, tunaangazia ngoma zinazotambaa kwenye mtandao wa YouTube Tanzania:

Soma Pia: Rayvanny Atajwa Msanii wa Pili Bongo Mwenye Mauzo Makubwa ya Muziki

Rostam ft Ferooz - Hujambo Mwanangu

Kwenye wimbo huu, Rostam wamemshirikisha msanii mwenzao maarufu Ferooz. Katika mistari yao, wanaangazia kazi aliyofanya hayati rais John Pombe Magufuli na rais wa sasa Samia Suluhu. Kufikia sasa wimbo huu una watazamaji zaidi ya laki nne.

Soma Pia: Wasifu wa Rose Muhando, Nyimbo Zake Bora, Albamu Zake, Tuzo Alizoshinda,Changamoto Alizopitia na Thamani Yake

https://www.youtube.com/watch?v=Ql4wkqmqyQ8

Do Lemme - Go MC Kinata ft Ibraah

Huu ni wimbo wa Singeli wake MC Kinata ambao alimshikisha Ibrah kutoka Konde Music Worldwide. Kwenye mistari yao Kinata, anaimba kuhusu upendo huku Ibraah akitupa michambo. Kufikia sasa ni wimbo ulio na watazamaji zaidi ya laki tano kwenye YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=uPU4Tjh1qSk

Kelebe – Rayvanny ft Innoss’B

Hii ni moja ya nyimbo zilizo kwenye alabamu yake Rayvvany ‘Sounds From Africa’. Wimbo huu umepokelewa vizuri huku wafuasi wakitengeza video fupi wakijitumbuiza na wimbo huu.

https://www.youtube.com/watch?v=V7sBxHz_nHE

Nobody - Anjella

Hii ni kazi yake Anjella kutoka Konde Gang iliyopokelewa kwa ukubwa sana. ‘Nobody’ ni wimbo wa mapenzi na kufikia sasa una watazamaji zaidi ya milioni mbili kwneye mtandao wa YouTube.

https://www.youtube.com/watch?v=-NCqC_BoUXc

Kiss Me – Mbosso

Huu ni wimbo wa mapenzi kutoka albamu ya Mbosso ‘Definition of Love’. Kwenye ngoma hii, ushairi wa Mbosso unajitokeza huku akisihi mpenzi wake ambusu.

https://www.youtube.com/watch?v=NpMXdlT3Cyc

Leave your comment