Wasifu wa Rose Muhando, Nyimbo Zake Bora, Albamu Zake, Tuzo Alizoshinda,Changamoto Alizopitia na Thamani Yake
17 May 2021
[Picha: Rose Muhando Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Rose Muhando ni nani?
Jina: Rose Muhando
Tarehe ya Kuzaliwa: Januari, 1976
Aina ya mziki: Mziki wa Injili
Thamani ya jumla: Haijulikani kwa sasa
Rose Muhando alizaliwa mwaka wa 1976 katika kijiji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania. Ni msanii maarufu wa muziki wa Injili katika lugha ya swahili.
Soma Pia: Nyimbo za Injili za Kiswahili Kwenye Mdundo (Pakua bila Malipo)
Awali, alikuwa mwimbaji mzuri sana wa kaswida,na alihudhuria kila siku madrasa huko Dumila morogoro kwani alikua muumini wa dini ya kiislamu. Baadaye, afya yake ilianza kudhoofika kutokana na ugonjwa ambao alihangaika kuupima. Aliteseka kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya hapo alipona na kubadili dini na kuwa Mkristo. Hapo ndipo alipoamua kwenda kanisani kwenye maombi.
Soma Pia: Wasifu wa Diamond Platnumz, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Thamani na Mahusiano Yake
Alianza fani yake ya muziki kama mwalimu wa kwaya inayoitwa Kwaya ya Mtakatifu Maria katika kanisa la kianglikana linaloitwa Chimuli mkoani Dodoma.
Rose Muhando ana tuzo ngapi?
Mnamo tarehe 31 mwezi Januari mwaka 2005, Rose Muhando alipata tuzo ya mtunzi bora, muimbaji bora, na tuzo ya msanii mwenye albamu bora ya mwaka wakati wa tamasha la tuzo za kiinjili, 2004.
Mwaka 2008 alipata Tuzo ya Mwimbaji bora zaidi wa Nyimbo za Injili Afrika zilizotolewa na Kenya Groove Awards.
Mwaka 2009, Rose Muhando alishinda Tuzo ya Mwimbaji bora zaidi wa Nyimbo za Injili Tanzania, na alishinda pia Tuzo ya Mwimbaji bora zaidi Tanzania na kuzawadiwa Sh200, 000 na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kupitia wimbo wake wa ‘Nibebe’.
Rose Muhando ana Albamu ngapi za mziki?
Baadhi ya albamu zake ni pamoja na:
- Kitimutimu.
- Uwe Macho, 2004.
- Jipange Sawasawa, 2008.
- Utamu wa Yesu 2011
- Yesu kun’guta, 2014
- Jitenge na Lutu 2017
- Miamba Imepasuka 2021
Nyimbo bora za Rose Muhando ni kama vile?
- Uwe macho
- Yes Nakupenda
- Jipange sawasawa
- Kenya Ulindwe
- Nakaza mwendo
- Hatumo
- Sitanyamaza
- Simba
- Wanyamazishe
- Miamba imepaasuka
- Kibembe
Maisha yake ya sasa yako vipi?
Kufikia mwaka 2018 Rose Muhando alipata matatizo mengi ya kiafya ambapo alilazimika kuenda Kenya kwa matibabu. Alipokosa namna ya kujilipia hela hizo, Rose Muhando alionekana katika kanda moja katika Kanisa la Neno Evangelism la muhubiri wa Kenya Pastor Ng’ang’a ambapo hali yake iliibua hisia mbali mbali kuhusu alichokua akipitia. Ilichukua hatua ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kushughulikia matibabu yake na kwa sasa yuko sawa.
Hivi karibuni alirudi kwenye ulingo wa mziki na albamu mpya “Miamba Imepasuka” na inaendelea kufanya vizuri sana.
Leave your comment