Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mpya ‘Kiss Me’

[Picha: Mbosso Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msani maarufu kutoka WCB Mbosso ameachia video ya wimbo wake ‘Kiss Me’.

Hii ni video ya nne kutoka kwa albamu yake ‘Definition of Love’ alioachia miezi miwili iliyopita.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Jux Adondosha Kanda ya Wimbo Mpya ‘Bado Yupo’

Katika kutafuta jibu ya nini maana ya mapenzi, ‘Kiss Me’ ni njia moja ambapo alipata ya kuonyesha upendo.

Katika mistari yake, Mbosso anaonyesha umahiri wake katika kuandika shairi la wimbo huu.

Anaanza kwa kueleza jinsi mpenzi wake humsifia kwa namna anavyompenda. “She says my love is original-ee (original),She says it's sweat and digital-ee (digital),My baby (koroga),My sweety (koroga),Nikupe tuzo mapenzi B.E.T (koroga),My darling (koroga),Oh, sweety…” aliimba Mbosso.

Soma Pia: Alikiba, K2ga na Samata Washirikiana kwa Wimbo Mpya ‘Nifuate’

Vile katika kanda hii tunawaona Mbosso na mrembo mmoja wakicheza. Wawili hao wanaonyesha uzuri ulioko kwenye mapenzi kupitia densi yao ya mabusu.

Michanganyiko ya mitindo ya kimavazi pia ni jambo nzuri hapa ambapo katika mikato ya video hii, tunawaona wawili hao na mavazi tofauti.

Kwa sasa, Mbosso anaonyesha uwezo wake kwa kuachia video hizi baada ya wiki mbili ili kuendelea kuafikia matakwa ya shabiki zake.

Wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube na zaidi ya watazamaji laki moja muda mchache baada ya kuachiwa.

Mdundo wa wimbo huu ulifanyiwa utayarishaji na Producer Kapipo wa Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=NpMXdlT3Cyc&ab_channel=Mbosso

Leave your comment