Alikiba, K2ga na Samata Washirikiana kwa Wimbo Mpya ‘Nifuate’

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii tajika wa muziki wa Bongo Fleva K2ga na mkurugenzi mkuu wa lebo ya Kings Music Alikiba wameachia ngoma mpya kwa jina ‘Nifuate’.

Huu ni wimbo unaozungumzia Tamasha la Nifuate ambalo limeanzishwa na Alikiba pamoja na mchezaji wa mpira Mbwana Samatta ambalo linatarajiwa kufanyika mwezi huu mkoani Iringa.

Katika ngoma hii zimesikika sauti za Alikiba pamoja na Samatta wakiwarai watu kujiunga nao katika kuendeleza kazi za kujitolea.

‘Nifuate’ ni mradi ambao wawili hao wanapania kutumia nafasi zao kukuza talanta za vijana.

 “…Pameshakucha, pamepambazuka ni kila mwaka kabumbu linachezeka, Nisamakiba nifuate imeshawaka team kiba team Samatta Nifuate…” aliimba K2ga.

Katika wimbo huu, K2ga anaendelea kudhihirisha ubabe wake kwa kutumia sauti yake vizuri.

Mistari ya wimbo huu pia haikua mingi hivyo uandishi wake haukua mgumu sana. Ukiskiliza wimbo huu maudhui yake ni ya kutaka kuskuma tamasha hilo.

Kwa muda mrefu, Alikiba amesema kama si mziki angekua mchezaji wa kandanda. Hivyo, tamasha hili linampa fursa ya kupea wengine nafasi ya kujimakinisha na talanta zao.

Samatta naye ni mchezaji maarufu kutoka Tanzania na kwa sasa anachezea Klabu ya Uturuki ya Fenerbahçe.

https://www.youtube.com/watch?v=B2ckrSU4yhQ&ab_channel=EnriqueIglesiasEnriqueIglesiasOfficialArtistChannel

Leave your comment