Producer Adam Juma Aonya Wasanii Dhidi ya Kudharau Radio na Televisheni Katika Sanaa Yao

[Picha: Simulizi na Sauti Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Mtayarishaji mkongwe wa video za muziki nchini Tanzania Adam Juma amewaonya wasanii dhidi ya kudharau vyombo vya habari kama redio na Televisheni kama kigezo cha kupeperusha kazi zao.

Soma Pia: Wasifu wa Rose Muhando, Nyimbo Zake Bora, Albamu Zake, Tuzo Alizoshinda,Changamoto Alizopitia na Thamani Yake

Akizungumza katika mahojiano, Adam amewasihi wasanii wa muziki haswa chipukizi kuzingatia sana kupeleka kazi zao redioni maana huko ndiko kwenye mashabiki wa kweli walipo.

“Kuna wengine hili swala la YouTube views ni biashara na inawalipa, views nyingi zinamlipa zaidi na haoni tabu kuinvest kwenye kuongeza kwa sababu soko lake linamruhusu kufanya hivyo,”alisema Adam.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: ‘Kelebe’ ya Rayvanny, Innoss’B na Ngoma Tano Zilizoachiwa Bongo Wiki

Vile vile, kupitia ukurasa wake wa Instagram, amefunguka kuwa kuna wasanii wakubwa wanaoweza jidai kwa kutumia YouTube views, lakini kwa wanaojitahidi kuchipuka ni hatari maana kuwa na YouTube views nyingi hazimaanishi kuwa nyimbo zako ndizo zinzovuma mtaani.

“Inasikitisha kweli kuona mtu ana views milioni mbili alafu Kigoma, Geita, Muheza huko nyimbo haijulikani. Kuna level ya msanii hizi views zinamsadia ila kwa wale chipukizi wanapotezwa vibaya sana kwa hii sura tunayoijenga kwenye tasnia. Ukweli unajulikana pale tu unaposimama kwenye stage sumbawanga alafu unaimba nyimbo yako yenye views 5.6m alafu mashabiki wanakuangalia tu. Wasanii msidhararu redio hasa hizi community radios ambazo zinawafikia watu moja kwa moja, tusiache kusambaza kazi zetu kutumia mifume ya ndani na nje mafanikio yatakuja tu,” aliandika Juma.

Adam alilazimika kuzungumzia swala hili baada ya madai kuwa wasanii wengine hununua views kwenye Youtube kuonyesha ukubwa wao katika mziki.

Leave your comment