Diamond Platnumz Kumshirikisha Focalistic Kwenye Albamu Yake

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii nguli wa Tanzania Diamond Platnumz anaendeleza shughuli yake ya kuanda albamu yake mpya nchini Afrika kusini. Diamond anatarajiwa kuwa huko kwa zaidi ya mwezi mmoja kwa ajili ya kazi hiyo nzima na shughuli mbali mbali ambazo hakuzitaja.

Pata Ubashiri wa Mechi Katika ya Real Madrid na Chelsea 

Katika vipengele vidogo vidogo kwenye mtandao wa Instagram Diamond ameweka video yake akiandaa albamu yake. Hivi karibuni aliweka video moja na msanii kutoka Afrika kusini Focalistic maarufu kwa wimbo wake ‘Ke star’ aliomshirikisha Davido wa Nigeria.

Fungu la Leo Zaburi 118:14

Video hii ilonyesha wawili hao katika harakati ya kutengeza wimbo ilio na mdudno wa Amapiano.

Hii ni moja tu ya video iliyoonyesha jinsi maandalizi ya albamu hiyo yanaendelea. Awali alionyesha kanda iliyokuwa na jina la Davido. Kanda hio ilizua gumzo kuwa msanii huyo atashirikishwa kwenye albamu hiyo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Zuchu, Rayvanny Waachia Ngoma Mbili Mpya Kwa Nina ‘Kazi Iendelee’

Diamond bado hajatangza jina au siku amabayo ataachia albamu hio inayosubiriwa na wengi barani Afrika.

Inatarajiwa kuwa albamu hii itakua na nyimbo mpya pekee na itatokea baadae mwakani.

Soma Pia: Wasifu wa Nandy, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake

Diamond ni mongoni mwa wasanii wengi nchini Tanzania wenye ahadi ya kuachia albamu mpya za mziki. Wasanii wengine wanaotarajiwa akuachia albamu zao ni kama vile Mausama, Lava lava, Marioo, Whozu, Moni Centrone, Killy na Cheed na Harmonize.

Leave your comment