Sikuwafunza Kupelekana Polisi: Diamond Awakashifu Rayvanny na Harmonize

[Picha: Diamond Platnumz Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Diamond Platnumz kwa mara ya kwanza amezungumzia zogo lilikuwepo kati ya Harmonize na Rayvanny. Alitoa ushauri kwa vijana wake hao kuhusu bifu za muziki akilinganisha na ile yake na mkurugenzi mkuu wa Kings Music Alikiba.

Katika mahojiano kupitia kipindi cha Refresh, Diamond ameonyesha kuchukizwa na mambo yanaoendelea kati ya msanii wake Rayvanny na aliyekuwa msani wake Harmonize kwa kupelekana polisi.

Soma Pia: Wasifu wa Diamond Platnumz, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Thamani na Mahusiano Yake

Diamond alieleza kuwa kile yeye alitaka kuona ni kuwa wanashindana kwenye kazi ya muziki . Alisisitiza kuwa hakuwafundisha kupelekana polisi.

“Sijui mara wamepelekana polisi mara nini….Sijafurahishwa kusikia wanapelekana Polisi, Waige mifano ya sisi kaka zao mfano mimi na Alikiba hatukuwahi kuepelekana polisi tulikuwa tunashindana kupitia kazi zetu tu.” alisema Diamond.

Soma Pia: Rayvanny vs Harmonize: Baba Levo Atozwa faini ya Tsh Milioni Moja Baada ya Kutoa Mwimbo Chafu.

Kwa sasa kesi ya Harmonize na Rayvanny ipo polisi kutokana na Harmonize kushtaki kuwa anachafuliwa kwa baadhi ya picha zake za utupu kusambaa mitandaoni.

Harmonize aliwashitaki wote waliohusika kusambaza hizo picha huku akiwashuku Rayvanny, Baba levo, Paula mtoto wa Kajala na Kajala mwenyewe.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021

Vile Vile Diamond Platnumz akiwa Afrika Kusini na producer @s2kizzy ameweka video katika Ukurasa wake wa Instagram Insta-Story ikionyesha wapo kwenye uandaaji wa album yake mpya.

Hata hivyo, Diamond bado hajaweka jina la albamu yake mpya na lini rasmi ataiachia.

Leave your comment