Rayvanny vs Harmonize: Baba Levo Atozwa faini ya Tsh Milioni Moja Baada ya Kutoa Mwimbo Chafu.
16 April 2021
[Picha: Babalevo Instagram]
Mwandishi: Branice Nafula
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram
Mwanamuziki Baba levo ametozwa faini ya shillingi milioni moja za Tanzania na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kumpa barua ya onyo kwa kosa la kusambaza wimbo wake kabla ya kuhakikiwa na baraza hilo.
Baada ya hapo Babalevo aliitwa kwenye kituo cha polisi cha Central ambapo bado hajataja mashtaka aliyoitiwa kule yeye na Rayvanny.
Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Tano Kali Kutoka Konde Music Worldwide Mwaka 2021
Alisema haya wakati akizinduliwa mbele ya wanahabari kuwa balozi wa kampuni ya kubashiri michezo.
Babalevo anasema kuitwa kwake BASATA ni kwa sababu ya wimbo wake alioachia bila ya kukaguliwa.
Wimbo huo uliojaa matusi kwa sasa umefungiwa.
“Jana kama mlivyoniona pale Basata niliitwa lakini kubwa ni kuhusu wimbo wangu ambao haukupitia taratibu katika kuutoa… tayari nimepokea barua ya onyo na kupigwa faini ya shilingi million moja,” alisema Babalevo.
SOMA PIA: Wasifu wa Rayvanny, Nyimbo Zake Bora, Tuzo Alizoshinda, Mahusiano na Thamani Yake
Aliongeza kuwa alitumwa na baraza hilo kupasha ujumbe kuwa hawataki mchezo na wala hawaogopi ukubwa wa jina ya msanii yeyote na atakayefanya makosa atachukuliwa hatua.
Hii ni kufautia kushtakiwa na Harmonize kuhusu zogo waliokua nayo na Rayvanny kwa ajila ya mwanawe Fridah Kajala. Katika mashtaka yake, Harmonize alisema kuwa Babalevo ni miongoni mwa waliohusika katika kusambaza picha chafu na sauti zinazomuhusisha yeye.
Aidha, amesema atakwenda mahakamani kudai fidia ya TZS milioni 6 kwa kuzushiwa kuwa amesambaza picha za utupu za Harmonize.
Leave your comment