Nyimbo Mpya: Young Killer Aachia Video Mpya Kwa Jina ‘Alhamdulilah’

[Picha:Young Killer Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Rapa kutoka Tanzania Young Killer ameachia wimbo mpya kwa jina ‘Alhamdulilah’.

Katika wimbo huu Killer anashukuru mashabiki kwa kumuunga mkono katika sana yake na biashara nyininezo.

Soma Pia: Tembo Vs Chui: Harmonize, Rayvanny Waachia Nyimbo Mpya ‘Vibaya’ na ‘Nyamaza’

Anaanza kwa kumshukuru mamake mzazi kwa kumlea na kumsapoti bila masharti.

“Eee Bwana, mama Msodoki see your boy, Kipenzi cha watu kinene wenye wanaenjoy, Shukran ziende kwa mwenyezi kwa haya mapenzi, wote walidhani siwezi…..” aliimba Young Killer.

Vile vile anaangazia safari yake alipoanzia mziki na jinsi alivyong’ang’ana kujijengea jina mjini Dar es Salaam kutoka Nyegezi.

Kwingineko anaichukua fursa ile kuwachamba wasanii wenzake waliomuona bwege .Anaongelea namna alihangaika kuandika mziki ila akadanganywa na kudharauliwa kwenye tamasha mbali mbali.

Soma Pia: Young Killer Aairisha Tarehe ya Kutoka kwa Albamu Yake

Young Killer anampa Mola shukrani kwa kufika alipo. Kanda ya wimbo hii inahisia mbalimbali tukimuona mamake mzazi katika tamasha moja akiwashukuru mashabiki kwa kumshabikia mwanawe.

Wimbo huu ulitengezwa na mtayarishaji wa mziki producer Dapro na video ikaelekezwa na Vass.

Wimbo huu ni mojawapo wa nyimbo kutoka albamu yake ya “The Riziki of Afrika” anayotarajiwa kuachia wakati wowote sasa.

Killer alilazimika kuarisha kuachia albamu yake kufuatia kifo cha aliyekuwa rais wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. Kufiki sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu kwenye mtandao wa YouTube na una watazamaji zaidi ya elfu sitini.

https://www.youtube.com/watch?v=A7sPMlwu47I&ab_channel=YoungKillerMsodoki

Leave your comment

Top stories

More News