Young Killer Aairisha Tarehe ya Kutoka kwa Albamu Yake

[Picha: Music in Africa]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii wa hip hop kutoka Tanzania Young Killer amesitisha uzinduzi wa albamu yake mpya iliotarajiwa kutoka mwezi Aprili tarehe 13.

Hii ni kufuatia kifo cha aliyekua rais wa Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Soma Pia: Pakua Mixtapes Tano Kali za Hip Hop Kutoka Bongo kwenye Mdundo

Alitangaza kusitishwa huko kupitia mtandao wake wa Instagram kuwa:

“Album postponed!! Napenda kuwatangizia kua Nimehairisha kutoka kwa album yangu kama nilivyoahidi mwaka jana. Kua album hiyo ingetoka tarehe 13 April 2021.Kufuatia msiba wa Kitaifa wa mpendwa wetu Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Natangaza kua album hii yenye viwango vya juu kabisa, Imesogezwa mbele mpaka hapo tarehe husika nyingine itakapo tangazwa.

Soma Pia: Tofauti Kati ya Muziki wa Asili wa TMK Wanaume na Kundi la Weusi

 

"Najua wapenzi wa mziki wangu na mashibiki zangu mli ngojea sana kwa hamu lakini najua kuwa nina watu wanao nipenda sana na wako tayari kuningojea. Hivyo basi tutaanza kuachia project hivi karibuni na Ninaahidi kuwafurahisha na kukata kiu yenu kwa kila kazi itakayotoka. Ninafurahi sana kuwa nanyi hapa. Ninawapenda,” aliandika Young Killer.

Vile vile ameahidi kuachia kazi mpya ili kuwafurahisha na kukata kiu ya mashabiki.

Young Killer ni mojawapo wa wasanii shupavu kutoka Bongo wanaofanya vyema sana. Albamu hii itakua ndio kazi yake ya kwanza mwaka huu na inatarajiwa kuwa bora zaidi.

Leave your comment

Top stories

More News