Tofauti Kati ya Muziki wa Asili wa TMK Wanaume na Kundi la Weusi

[Image Source: Mtikiso Entertainment]

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Fani ya muziki wa hip hop  nchini Tanzania imekuwa ikibadilika kwa miaka mingi. Awali muziki wa hip hop wa Tanzania ulikuwa wa Bongo Flava asili.

 Waliotambulika katika mziki hii walikua TMK Wanaume original, Dog Malik, JCB, Watengwa,Chindo aka Umbwax, Donii, Wadudu wa dampo, Jambo Squad, Gnako, Weusi, na wengineo.

Soma Pia: Pakua Mixtapes Tano Kali za Hip Hop Kutoka Bongo kwenye Mdundo

 Rapa wa Tanzania waliangazia kile walichokiona karibu yao. Maudhui yao nyimbo  yakiwa juu ya umasikini, hatari za HIV, rushwa na ugumu wa jumla wa kukulia katika taifa linaloendelea wakati ule.

Huku tukijaribu kuangazia ukuaji wa mziki huu wa hip hop, katika nakala hii tunaangazia tofauti ulioko kati ya mziki wa awali wa TMK Wanaume halisi na kundi la Weusi. 

Uhalisi

Tmk Wanaume waliangazia kwa wingi mambo yaliyo wahusu wao kam wasanii na jamii kwa ujumla. Wimbo kama vil;e “Kichwa kinauma” uliongazia bidii yao kazini huku mapatao yakiwa madogo sana. Kwingineko Weusi mziki wao kwa wingi uliangazia mapenzi na maudhui mengine.

https://www.youtube.com/watch?v=C6YLxJ4v7uA

Mtindo

Awali wanamziki wa Tmk walitumia mdundo wa kasi kiaisi katika uimbaji na mtindo wao wa rap mfano ukiwa wimbo wa “Dar Mpaka Moro” . Huku Kundi la Weusi likiongozwa na Joh Makini wakichukua mtindo wa pole kupiga rap kwa mtindo wa pole pole kiasi.

https://www.youtube.com/watch?v=UTUkFDdYrj4

 Ukuaji

Ukuaji wa mfumo wa kidijitali umesadia bendi ya Weusi amabayo imebaki kuwa timu licha ya kuwa na taaluma ya muziki kibinafsi. Hivyo wasanii kama Gnako   na  Joh Makini wanatambulika kwa kazi zao wanazoeka kwenye kurasa zao za mziki. Hii ikiwa tofauti na TMK Wanaume ambao walisambaratika miaka michache iliyopita na wanajaribu kurudi kufanya kazi pamoja tena.

https://www.youtube.com/watch?v=n6Cg9Irdemk

Umoja

TMK Wanaume kwa sasa ni kundi la kutamaniwa tu huku masahabiki wakiendelea  kuskiza nyimbo zao za kitambo na tumaina la kundi hilo kurudi kufanya kazi pamoja. Tofauti na ilivyo kwenye kundi la Weusi ambapo licha ya baadhi yao kuwa na kazi zao za kibanfsi wao huungana na kuachia kazi ya pamoja. Hivi karibuni Kundi la Weusi wameachia albamu yao mpya iitwayo  “Air Weusi”  ambayo inaendelea kufanya vizuri .

 

Leave your comment