BaikokoChallenge: Video Tano za Densi ya Wimbo wa Mbosso ‘Baikoko’ Zinazovuma

[Picha: Mbosso Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Wiki chache baada ya Mbosso kuachia wimbo wake wa Baikoko akimshirikisha Diamond, mashabaki nao hawajachelewa katika kupokea wimbo huu kwa kufanya #Baikokodance Challenge.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso Aachia Video Mpya Kwa Jina 'Yalah'

Wakati mahsabiki wanaendelea kusubiria kanda ya nyimbo hio, wengi walipata fursa ya kuonyesha upendo wao kwa challenge hii.

Baikokodance Challenge inakuwa Challenge kubwa ya densi mwaka huu haswa kwa wimbo ambao hauna video kwa sasa.

Soma Pia: Zuchu Aweka Rekodi Mpya YouTube Tanzania

Hivyo tuangizie Video Tano za mashabiki walio furahishwa na wimbo huu.

Angel Nyigu kutoka Tanzania

Huyu ni mojawapo wa wasakataji wa nyimbo nyingi za Wasafi. Angel Nyigu na rafiki zake watatu ndio waanzilishi wa challenge hii ambayo kwa sasa imekubalika na wanaTiKTok wote. 

https://www.instagram.com/p/CMcNhuyHCBS/?utm_source=ig_web_copy_link

Azziad Nasenya na wenzake kutoka Kenya

Msakataji densi kutoka Kenya Azziad Nasenya hakuachwa nyuma katika challenge hii. Yeye na wenzake walionekana kufurahia wimbo huu. Video yao imesamba dhihirisho kuwa imewafurahisha wengi mtandaoni.

https://www.instagram.com/p/CM-WYwCnPvF/?utm_source=ig_web_copy_link

Im River Flows Kutoka Norway

Huyu alirukia wimbo huu kutoka Norway kuonyesha ushabikiaji wake kwa mziki wa Tanzania. Im River Flows ni mwenye asili ya Tanzania ni mkaazi kule Norway. 

https://www.instagram.com/p/CMhBV9yA558/?utm_source=ig_web_copy_link

Karina Palma wa Dubai

Huyu ni mwanadensi ambaye anajulikana kwa kuenzi mziki wa Tanzania hivyo anaonekana akicheza wimbo wa Baikoko kwa ujuzi mkubwa.

https://www.instagram.com/p/CNA1bNTnSDI/?utm_source=ig_web_copy_link

Mulamwah kutoka Kenya

Mchekeshaji kutoka Kenya almaarufu Mulamwah alionekana kurukia challenge hii ambapo alionyesha ubabe wake katika usakataji akiwa na mwenzake Bree Jonhsons.

https://www.instagram.com/p/CM-X1RqncRu/?utm_source=ig_web_copy_link

Leave your comment