Nyimbo Mpya:Tanzania All stars Waachia Video ya Wimbo Wao “Lala Salama”

Mwandishi:Branice Nafula

Wakati nchi nzima ya Tanzania inaendelea kumboleza kifo cha hayati Rais John Pombe Magufuli, Wasanii mbali mbali walijitokeza kumuomboleza rais huyo kwa kutunga nyimbo za kumbukizi.

Hivyo wasanii tajika toka Tanzania almaarufu Tanzania all Stars wameachia kanda ya wimbo wao “Lala Salama”.

Wimbo huu umejaa majonzi,simanzi na ufundi kwa pamoja. Mbosso anaanza wimbo huu kwa kuangazia machungu waliyonayo watanzania kwa kumpoteza kiongozi wao ghafla.

“Nalifuta chozi kushoto Kulia latiririka Maumivu moyo wa moto Nafsi yatatarika Vilio wakubwa watoto Viyowe we zinasikikika Wachonge zetu changamoto Wapi zitashikika…” aliimba Mbosso.

Join Us on Telegram

Kisha Christina Shusho anaingia kwa kumuaga rais huyo. Vile vile Jux naye anaahidi kuwa Tanzania itamkumbuka Magufuli kwa upendo wake.
Kwa kifupi wasanii wengine husika katika wimbo huu ni kama vile Diamond Platnumz, Juma Jux,Rayvanny, Madee, BI.Khadija Kopa, Zuchu,Gnako,Lavalava, Babalevo,Dula Makabilla, Joel Lwaga, Aby Chams, Belle 9, Maarafia,QueenDarleen,Mrisho Mpoto,Chege, Mrisho Mpoto,Mausama, BenPol, Karen miongoni mwa wengine wengi..

Kanda hii imetengezwa kwa ujuzi wa director Kenny huku, wimbo wenyewe ukitengezwa na watayarishaji mashuhuri wa mziki wakiwemo Lizer Classic, S2Kizzy, Abbah na Trone.

Katika kuumpa heshima hayati rais Magufuli watayarishaji hao walisema kazi hii waliifanya bila ya kutarajia malipo yoyote.
Kufikia sasa huu ni wimbo mojawapo unaotumika katika hafla nzima ya kumuomboleza rais huyo.Dhihirisho la umoja wa wananchi wa Tanzania.

 

Download Diamond Platnumz Music FREE

https://www.youtube.com/watch?v=gD-VdBqHscY&ab_channel=Harmonize

 

Leave your comment