Nyimbo Mpya: Abdukiba Amshirikisha Singah Katika Wimbo Mpya ‘Give More’

[Picha: Abdukiba Instagram]

Mwandishi: Branice Nafula

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Bure Kwenye Telegram

Msanii kutoka lebo ya Kings Music Records Abdukiba ameachia wimbo wake mpya kwa jina ‘Give More’.

Katika wimbo huu, Abdukiba amemshirikisha msanii kutoka Nigeria Singah ambaye anasifika kwa kazi yake nzuri.

Soma Pia: Soma Pia: Nyimbo Mpya: Ngoma Zake Nandy Zinazovuma Bongo

Huu ni wimbo mzuri wa upendo ambapo mwanamume mmoja anamsifia msichana wake jinsi anavyocheza.

“Eyoo, girls show me how you love me more, I wanna show you more and more na nishaweka kando wanaojipa promo hainipimi kipimo.Hello babay naitest one time girl,twende chini vuta pumzi niachie ma...” hii ni baadhi ya mistari kwenye wimbo huu.

Wakati Abdukiba anasifia mpenzi wake anavyocheza, Singah anaingia na kumuomba dada yule asimnyime upendo huo.

Soma Pia: Nyimbo Mpya: Mbosso, Anjella Wang'aa Kwenye Nyimbo Tano Bora Wiki Hii

Wawili hawa wamedhihirisha ufundi wao katika kuachia mziki wenye mdundo wa densi na kanda ya wimbo huu pia ilandaliwa vizuri.

Ukiangalia wahusika na kundi la wasakataji densi ambao wanatambua kilichohitajika kwenye wimbo wa ‘Give more’.

Kufikia sasa wimbo huu unaendelea kupata umaarufu zaidi kwenye mtandao wa YouTube na watazamaji zaidi ya elfu sitini na tisa. Video ya Muziki ilipigwa Dar es Salaam, Iliyoongozwa na muelekezaji maarufu Elvis huku mdundo ukiandaliwa na Mocco Genius.

https://www.youtube.com/watch?v=iOzNFo1RDR4

Leave your comment